
Mgombea Urais kwa tiketi ya CUF ambae ni Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi Fomu za Urais Afisa wa tume ya Uchaguzi ZEC leo akimaanisha kukamilisha masharti yote aliyotakiwa kuyatimiza.

Maalim Seif Sharif Hamad akitia saini katika kitabu cha Tume.

Baadhi ya viongozi waandamizi pamoja na wanachama wa CUF waliomsindikiza Maalim Seif Sharif Hamad wakishuhudia urudishwaji wa Fomu hizo.

Maalim Seif Sharif Hamad akiongea na waandishi wa habari baada ya kurudisha fomu za kugombea Urais Zanzibar.

Waandishi tofauti wakimhoji Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kurejesha Fomu zake Tume.
No comments:
Post a Comment