Habari za Punde

RAIS KARUME AENDELEA NA ZIARA - NAMIBIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akitoa maelekezo kwa Waziri wa nchi Afisi ya Rais Fedha na Uchumi Mwinyihaji Makame,(kulia), katikati ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya mashariki Mohammed
Aboud, nje ya ukumbi wa mkutano wa SADC Safari Court Hotel, Namibia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume (kulia) akiongozana na Maofisa akielekea katika Ukumbi wa Mkutano wa nchi za SADC unaoendelea Nchini Namibia leo, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Washiriki wa mkutano wa SADC kutoka Nchini Tanzania wakifuatilia kwa makini harakati za mkutano huo unaofanyika nchini Namibia ambayo ndio imeshika nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC unaodumu kwa muda wa mwaka mmoja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akisalimiana na Waziri wa Mazingira na Utalii wa nchini Namibia, Mama Mitumbo Ndaitwa, wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa nchi hiyo juzi, katika ziara hiyo amefuatana na Mkewe Mama Shadya Karume.
Picha na Ramadhan Othman, Namibia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.