Habari za Punde

"SHIBORI" APATA MAUMIVU YA KIUNO


Ashauriwa kupumzika mwezi mmoja

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes ambaye ni mchezaji aliyesajiliwa na Simba ya Dar katika dirisha dogo la usajili alipata maumivu hayo wakati akiwa  katika mazoezi na Timu ya Taifa.

Shibori aliyaanza mashindano hayo kwa kupachika mabao mawili katika mchezo wa fungua dimba na Sudan, alishindwa kufurukuta katika mechi ya pili dhidi ya Ivory Coast ambapo alipumzishwa katika kipindi cha pili.

Katika mechi ya mwisho alikuwa tayari majeruhi kwa hivyo hakuonekana uwanjani dhidi ya Waganda.

Ally Ahmed Shibori ametokea timu ya Duma na katika msimu uliopita aliweza kupachika magoli 15 katika ligi ya Zanzibar jambo liliwavutia timu za Simba na Yanga kutaka saini yake na hatimae Simba kuweza kuibuka kidedea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.