Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes imefanikiwa kuingia katika robo fainali ya Kombe La Challenge baada ya kuwa ni mojawapo ya timu bora (best loser). Katika mchezo wa mwisho wa kundi lake , Ivory Coast iliifunga Sudan 3-0 na hivyo Ivory Coast kuongoza kwa pointi 7 na kufuatiwa na Rwanda pointi tano na kisha Zanzibar pointi nne.
Zanzibar Heroes imeungana na Burundi kama timu bora na hivyo imepangiwa kucheza na Timu ya Taifa ya Uganda, the Cranes, bingwa mtetezi.
Kocha Stewart Hall amefarijika kwa kuweza kuvuka katika kundi gumu lililopewa jina Kundi la Kifo na kwa kupata muda mzuri wa mapumziko atahakikisha anawaandaa wachezaji wake vizuri katika kukabliana na Waganda katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 8, Uwanja wa Taifa.
“Kuna mengi niliyoyaona katika hatua ya makundi na tayari nimeshaanza kuyafanyika kazi ili ndoto zetu ziweze kutimia kama tulivyopanga,” alisema Hall
Zanzibar Heroes ilianza mashindano kwa kishindo kwa kuifunga Sudan 2-0 na kisha kupoteza mchezo wake dhidi ya Ivory Coast 1-0 na kumalizia kwa sare ya 0-0 na Rwanda.
Katika mtanange kama huu mwaka uliopita Zanzibar Heroes ilifungwa na Uganda 2-1.
Blog yako inawapongeza wachezaji wote wa Zanzibar Heroes na kuwatakia kila la kheri katika mchezo wao na timu ngumu ya Uganda ambayo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote
Blog yako inawapongeza wachezaji wote wa Zanzibar Heroes na kuwatakia kila la kheri katika mchezo wao na timu ngumu ya Uganda ambayo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote
No comments:
Post a Comment