Habari za Punde

DAWA YA KUONDOA MSONGAMANO BARABARA YA DARAJANI

Barabara ya Darajani ndio imekuwa barabara kuu na kila magari yakiongezeka imekuwa ikisababibisha usumbufu wa foleni kwa kutumika kwa magari, daladala, magari ya mizigo, magari ya watalii, baskeli, pikipiki na hata waenda kwa miguu.

Mara ya mwisho kufanyiwa ukarabati ni takriban miaka kumi iliyopita na ushee hivyo maoni yangu ni kwamba barabara hii iwe dual carriage way iwe ya na njia nne badala ya mbili zilizopo na kunaweza kumegwa sehemu ya viwanja vya Malindi na maduka ya Vioo Darajani kuvunjwa kwani sehemu pekee ambayo ina majengo katika kupitisha barabara hii ambapo kwengine ni Bustani ya Jamhuri na sehemu za viwanja vya Mnazi mmoja.

Pia katika ujenzi huu kunaweza kuwekwa njia za wanaokwenda kwa miguu na hata waendesha baskeli ili kuweza kupunguza msongamano na ajali.

Ni mtazamo tu 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.