Habari za Punde

MAKAMO WA RAIS ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA JAPAN

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu kufuatia maafa makubwa yaliyotokana na Tsunami Nchini Japan hivi karibuni, wakati alipokwenda katika Ofisi za Ubalozi huo Upanga jijini Dar es salaam leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa wakati alipokwenda kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Japan Upanga jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu kutokana na maafa makubwa yaliyotokana na Sunami Nchini Japan hivi karibuni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa wakati alipokwenda kwenye Ofisi za Ubalozi wa Japan  Upanga jijini Dar es salaam leo, kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu kufuatia maafa makubwa yaliyotokea Nchini Japan hivi karibuni yaliyosababishwa na Tsunami.

Picha na Amour Nassor VPO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.