Habari za Punde

HUMOUD - USHAROBOLO SASA BASI

 Jackson Odoyo

KIUNGO mpya wa Azam, Abdulhalim Humoud amesema hana mpango tena wa kuishi maisha ya kisharobalo badala yake ameamua kumrudia Muumba wake kwa kupiga swala tano kila siku.

Humoud aliyeshindwa kutamba ndani ya Simba amejiunga na Azam na kusaini mkataba mnono zaidi ya alikuwa akipata kutoka kwa vijana wa Msimbazi.

Akizungumza na Mwanachi jana Humoud ambaye aliwahi kutangaza kuwa yuko tayari kuhamia Yanga hata bure kutokana na kuchoshwa na manyanyaso ndani ya Simba alisema amefikia uamuzi huo wa kuachana na tabia za masharobaro kwa sababu hakuona faida yake.

Hivi sasa mimi ni Humoud mpya si yule aliyekuwa akisuka akiwa Mtibwa wala yule aliyekuwa akijichora mwili msima, hivi sasa mimi ni mswalina wa swala tano na baada ya suala tano ninaingia kulala kabla ya muda wangu wa mazoezi kufika,îalisema kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.

Alisema ingawa anaweza asinyoe nywele zake, lakini kamwe hata suka tena wala hatajipiga mikorogo na wala hata paka rangi na michoro ya ajabu mwilini mwake kwa sababu amebaini kuwa hata Mwenyezi Mungu hapendi mambo hayo.

Kuhusu nafasi ya kuitumikia klabu yake mpya alisema kuwa ndani ya Azam kuna changamoto kubwa kwa sababu hivi sasa ni timu kubwa na inawachezaji wazuri hivyo atajitahidi kufanya mazoezi ya nguvu na kujituma uwanjani kila atakapokuwa anapewa nafasi ya kucheza.

Huu ni wakati wangu wa kufanya kazi na cha msingi ninahitaji kurejea timu ya taifa hivyo ni lazima nifanye kazi ya maana ndani ya Azam ili nipate kibali cha kurejea timu ya taifa taifa Stars kwani huwezi kuitwa timu ya taifa kama hauna mchango katika klabu yako alifafanua kiungo huyo.

Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.