JUMLA ya shilingi milioni tisa zimetumika katika kukamilisha miradi sita kwenye wadi mbalimbali za halmashauri ya wilaya ya Magharibi kwa lengo kukuza maendeleo kwenye wadi hizo.
Katibu wa halmashauri hiyo Bakari Khatib Shaaban, alieleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mombasa nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Alisema fedha hizo zimetumika katika wadi sita tofauti za wilaya hiyo zikiwemo Kizimbani ambapo halmashauri ilichangia ujenzi wa skuli ya Chekechea, huku wadi za Dolem Mwera halmashauri hiyo ilichangia ujenzi wa hospitali.
Aidha alisema fedha hizo pia ilichangia katika wadi ya Dimani katika ujenzi wa skuli ya Bwefumu na ujenzi wa skuli wadi ya Bububu utiaji wa kifusi wadi ya Uwelezo.
Alifafanua kuwa utaratibu huo wameueka kwa lengo la kusaidia maendeleo ya wana jamii ambayo miradi hupitishwa na madiwani waliyopo katika wilaya hiyo ili kuondokana na hali ngumu ya kimaisha inayowakabili wananchi.
Aidha alifahamisha kuwa kama mipango itakwenda vizuri wanategemea mwezi wa sita kuwanza kutekeleza miradi iliyo bakia katika wadi mbali mbali za wilaya hiyo.
Hata hivyo aliwataka wananchi wawe na mashirikiano ya hali ya pamoja na ulipaji wa ada mbali mbali zinazo kusanywa na halimashauri kwalengo lakuyatatua matatizo ya wananchi kwa njia rahisi zaidi.
No comments:
Post a Comment