Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,akiwapa pole wananchi wa wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,waliofiliwa na jamaa zao katika tukiokubwa la kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika mkondo wa Nungwi,huko uwanja wa Gombani jana,katika ziara maalum ya kuwapapole wafiwa kisiwani Pemba.
Wananchi wa Wilaya ya Chake chake Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa na mazungumzo na wananchi hao, katika uwanja wa Gombani, alipowapa pole ya kufiliwa na jamaa zao,kutokana na jamaa zao kwa ajali ya kuzama meli ya Mv Spice Islander,huko katika mkondo wa Nungwi hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwafariji wananchi waliofiliwa na jamaa zao, katika ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander huko mkondo wa Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja, hivi karibuni, akiwa katika ziara kuwafariji wananchi katika ukumbi wa umoja ni nguvu Mkoani Pemba
Wananchi wa wilaya ya Mkoani Pemba,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander, iliyotokea wiki iliyopita katika mkondo wa Nungwi, kaskazini Unguja,wakiitikia dua iliyoombwa na sheikh Hamadi Juma,baada ya mazungumzo na Rais wa Zanzibar alipofika kuwapa pole katika ukumbi wa umoja ni nguvu Mkoani Pemba
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,pamoja na wananchi waliofiliwa na ndugu zao katika Ajali ya meli ya Mv Spice Islander, katika mkondo wa Nungwi, wakiitikia dua baada ya kuwapa pole alipofanya nao mazungumzo,na kuwataka kuwa na subira kwani hiyo ni kazi ya Mungu, katika ukumbi wa Umoja ni Nguvu Mkoani Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi waliofiliwa na ndugu zao katika Ajali ya meli ya Mv Spice Islander, katika mkondo wa Nungwi, mazungumzo hayo yalifanyika jana katika ukumbi wa Umoja ni Nguvu Mkoani Pemba
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na viongozi wa pamoja na wananchi waliofika katika mapokezi alipowasili uwanja wa karume Pemba, akiwa katika ziara ya kuwafariji wananchi kisiwani Pemba waliofliwa na jamaa zao katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander Hivi Karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Jabu Khamis Mbwana akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipofika kutowa mkono wa pole kwa Wananchi waliofiwa na jamaazao katika ukumbi wa Umoja Mkoani
Picha zote na Ramadhan Othman, Pemba
No comments:
Post a Comment