Habari za Punde

DK SHEIN AWAAPISHA MAKAMISHNA, VIONGOZI WA DINI

Na Rajab Mkasaba, Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amewaapisha viongozi mbali mbali akiwemo Sheikh Saleh Omar Kabhi kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar jana.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud,Mawaziri, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdala Mwinyi, Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibaribar na viongozi wengine.


Dk. Shein pia, amemuapisha Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Wengine ni Muumin Khamis Kombo aliyeapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Abdulrahman Mwinyijumbe kuwa Mshauri wa Rais Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Dk. Shein pia, amemuapisha Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa kuwa Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji, Burhan Saadat Haji kuwa Mshauri wa Rais Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi ambapo Issa Ahmed Othman amemuapisha kuwa Mshauri wa Rais Utalii.

Aidha, Dk. Shein amemuapisha Mohammed Fakih Mohammed kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, Jaji Hamid Mahmod Hamid, Mabrouk Jabu Makame, Issa Mohammed Suleiman, Ali Rajab Juma, Balozi Hussein Said Khatib na Jecha Salim Jecha ambao wote wameapishwa kuwa Wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.

Wakati huo huo, Rais Dk. Shein amempandisha Cheo Naibu Kamishna Khalifa Hassan Choum kuwa Kamishna kabla ya kumuapisha kuwa Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.