Habari za Punde

SALAMU KUTOKA KWA DA SUBI

Mwanablogu mwenzangu,

Ndugu yangu Othman Maulid,

Nakuandikia kukupa pole kwa msiba uliotufika sote kama taifa lakini sana kwako na watu wote wa Zanzibar kufuatia ajali ya meli ya Spice Islander.
Ni vigumu kuweza kutoa pole ya kupoza machungu yaliyotokea.
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ushupavu na uhodari ulioutia katika kupasha habari za tukio hili tangu awali hadi sasa.
Umeuwezesha umma wa ulimwengu mzima kuona kwa njia ya maandishi na picha kile kilichokuwa kinaendelea.
Umekuwa kiungo muhimu pale ambapo yalikuwepo mapungufu ya upatikanaji habari hii.

Mimi pamoja na wenzangu tulio wengi tunakushukuru na kukutakia afya njema na heri nyingi ili uendelee kufanikisha kazi hii ya upashaji habari.

Asante kwa kutembelea wavuti.com kila unapopata nafasi, nami napenda kukufahamisha kuwa ni 'subscriber' wa blogu yako kwa njia ya RSS, napata 'updates' zote unazoziweka na kuzituma kwa wengine wanaofuatilia na kupenda kufahamu yanayotukia Zanzibar.

Nakutakia kila la heri!

Subi|wavuti.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.