Habari za Punde

WAJUMBE WA TUME YA UTAWALA BORA ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, amefanya uteuzi wa Tume ya Utumishi Serikalini Zanzibar.

Katika uteuzi huo, amemteua Othman Bakari Othmani kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, kabla ya hapo ndugu Othman Bakari Othman alikuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Pia amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Tume hiyo.

Walioteuliwa ni Rabia M Hamdani, Fatma Mohamed Othman, Salama Kombo, Yussuf Ali Salim, Salmin Senga Salmin na Juma Haji Juma.

Uteuzi huo umeanza tarehe 7 Mwezi huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.