Na Mwantanga Ame
SERIKALI ya Zanzibar inajiandaa kuweka kanuni itayoweza kudhibiti uingiaji wa bidhaa chakavu pamoja na uuzwaji, uangamizaji wa bidhaa za aina hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej aliyasema hayo jana wakati akijibu suali la Rufai Said Rufai (Tumbe) alietaka kujua ni hatua gani serikali imejiandaa kudhibiti tatizo la uingiaji wa vitu chakavu ili kunusuru vizazi vijavyo.
Waziri huyo alisema serikali imelazimika kuandaa kanuni hizo kutokana na kuonekana kumekuwa na ongezeko kubwa la uingiaji wa vifaa hivyo huku ikiwa inakosa njia mbadala katika kukabiliana na athari za kimazingira zitazotokana na taka za vitu hivyo.
Alisema Wizara yake tayari inaandaa kanuni hizo baada ya kupata maoni kutoka kwa wataalamu wa Mazingira ambao walilifanyia utafiti suala hilo na kutoa mapendekezo mbali mbali juu ya hatua za kuchukuliwa katika kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema hivi sasa Zanzibar imekuwa ikipokea makontena 23,000 na asilimia 20 huingiza bidhaa chakavu kwa kila mwaka kiwango ambacho hufikia asilimia 99.360 bidhaa chakavu
Tume ya Utangazaji alisema Waziri huyo kwamba hivi sasa ina vifaa vya Televisheni 300,000 na redio 11,000 ambavyo vinahitaji kuangamizwa lakini bado hawaju wapi wataweza kutupa vifaa hivyo.
Alisema vifaa ambavyo tayari vimekuwa vikiingizwa ambavyo ni chakavu ni pamoja na Kompyuta, mafriji, simu, pasi, televisheni na redio ambapo imebainika kuwa na madini makali aina ya Lead, Mercury na Caldium yanayoweza kuleta athari za kiafya ukiwemo ugonjwa wa saratani na kuathiri viumbe vyengine.
Waziri huyo alisema kuwa katika kukabiliana na tatizo hilo Wizara inatarajia kukamilisha kanuni hiyo ifikapo Mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni hatua ya kusaidia Zanzibar kuwa salama na bidhaa chakavu kwa faida ya vizazi vijavyo.
Sambamba na hilo Waziri huyo alisema kanuni hiyo pia itaweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara kwa wananchi wanayoweza kuyapata juu ya utumiaji wa vifaa hivyo.
"....Wizara inatarajia kukamilisha kanuni hiyo ifikapo mwezi September mwa huu..."!!!!!!!
ReplyDeletehapo naona sijui mwandishi kakosea au ndivyo alivyosema?!!!!
Nadhani ni kuteleza kwani Septemba imeshapita iliyokusudiwa ijayo.
ReplyDeleteHatukatai kuwa asilimia fulani ya vitu vinavyoletwa na ndugu zetu walioko nje ni chakavu na ni uharibifu wa mazingira lakini serikali pia izitupie macho bidhaa ambazo zinaletwa kutoka China.Kwa kweli asilimia fulani ya bidhaa hizo ni chakavu kuliko hata hizo zinazoletwa na ndugu zetu kutoka Ulaya.Wananchi wetu wanadanganyika na upya wa bidhaa hizo,haiwezekani kitu umekinunua leo baada ya wiki au mwezi kimekufa.Sasa jee ikiwa hali tutaachia hivyo kwa vitu ambavyo havina viwango kwasababu tu vimetoka kwa marafiki zetu wa kichina mnategemea visiwa vyetu vitakuwa vipi kimazingira baada ya miaka michache ijayo?
ReplyDeleteHaya mjadili unazidi kunoga ikiwa hivi used vitapigwa na marufuku na vipya fake vya Mchina vipigwe marufuku mwananchi wa kawaida itambidi ajibane kweli kweli mpaka aweze kununua angalau kafriji cha kupata maji baridi na kuhifadhi vitoweo.
ReplyDeleteTujifunze kwa nchi zilizokataza used kama Uganda na kwengineko.
Tatizo viongozi wetu wanakurupuka, madam sisi ni maskini vitu chakavu na vile feki vya kichina hatuwezi kuviepuka..tusiige watu! Kuna waziri mmoja wa afya wa SMZ(sasa hivi maremu) yeye alikurupukaia kupiga marifuku uingizaji wa mitumba..ama yeye mwenyewe ndio iliyo msitiri kabla hajafa,kwa vile hakua waziri tena na aliishia upinzani. Tuweni wakweli jamani.
ReplyDelete