Habari za Punde

KWA WAWAKILISHI - NAOMBA MKANIULIZIE SUALI

Assalaamu 'Alaykum

Kama wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanabahatika kupitia kwenye blog hii nawaomba wakaniulizie suala langu Barazani kuhusiana na uchache wa madaktari na mainjinia wakati kulikuwa na program maalum ya Islamic Development Bank (IDB) kuanzia miaka ya themanini ambapo ililenga katika kuinua uwezo wa wazanzibari katika nyanja hii kwa kutoa scholarship maalum za kuwapeleka watoto wetu katika nchi ya Uturuki kusomea udaktari au mambo ya technology.

Walikuwa wanatagemewa wakimaliza masomo wangerudi nchini kuja kusaidia sekta hizi na kuinua hali ya uchumi katika upande wa teknolojia na pia katika sekta ya afya.

Je Serikali ina Data zinazoonesha ni wanafunzi wengapi walionufaika na scholarshipi hizi mpaka sasa na wengapi wamerudi nchini na wengapi hawakurudi?

Kuna wale waliorudi na kisha kuondoka kwenda kutafuta maslahi bora na je serikali ina idadi yao pia?

Tunao kina Profesa Idris Rai ambae ni Makamu wa Chuo kikuu cha Suza, Dr Nawfal Kassim ambaye yupo Mnazimmoja na pia ni katibu wa Zanzibar Outreach Program na kuna na wengine wengi wakiwa ni matunda ya Program hizi kwa kuonesha mifano tu.

Kutoka Kwa Mdau - Uingereza

1 comment:

  1. Ndugu yangu, nakupongeza kwa changamoto uliyoitoa. lakini sidhani kama kuna mwakilishi anaetembelea mtandao, achilia mbali huu wa Mapara. Mw.nyerere alisema Watanzania hatuna utamaduni wa kusoma lkn. nadhani sisi Wazenj tumezidi. hivi unaamini kuwa kuna baadhi ya wawakilishi badala ya kuulizia mambo kama hayo uliyoyataja badala yake wanaulizia mipango ya serekali ktk kuwajengea nyumba wafanyakazi wake huku hali ya uchumi wanaiona! Hao vijana uiowataja inaonyesha wapo ila hatujui wapi? Nilipokua mwanafunzi miaka ya 90 nilisikia kijana mmoja akitajwa sana kama'khatib mwamba' na ambae nilisikia alikwenda Uturuki.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.