NDEGE iliomchukuwa Mwana wa Malkia wa Uingereza ikiwasili Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
MWANA wa Malkia wa Uingereza, Prince Charles, akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar pamoja na Mkewe Bi Camilla kwa ziara ya siku moja katika kisiwa wa Unguja.
Mwana wa Malkia wa Uingereza akiwasalimia Watoto Hafsa Hamad na Zahira Mussa, baada ya kuvalishwa mauwa alipowasili Zanzibar Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, kwa ziara ya siku moja.
MWANA wa Malkia wa Uingereza akisalimiana na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Mwana wa Malkia wa Uingereza akisalimiana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi Zanzibar.
MWANA wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles, akiangalia Ngoma ya Mwanandege alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar.
MSANII wa Kikundi cha Sanaa Zanzibar Boha akicheza ngoma ya Kibati.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mama Mwanamwema Shein (kulia) Mama Asha Balozi Seif na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame.
UJUMBE wa msafara wa Mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles, wakiwa Ikulu ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mahamed Shein, akimkabidhi zawadi Mwana wa Mfalme Prince Charles, alipofika Ikulu kuonana na Rais wa Zanzibar, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Prince Charles Camilla.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi zawadi Mke wa Mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles Camalli.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi zawadi Mke wa Mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles Camalli.
MKE wa Mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles Camilla, akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein.Ikulu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na mgeni wake akiangalia Kasha la njumu, baada ya kumkabidhi zawadi .
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Mwana wa Mfalme Prince Charles, Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Prince Charles Camilla.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Mwana wa Mfalme Prince Charles, Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Asha Balozi na Mke wa Prince Charles Camilla. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,
GARI lilomchukwa Mwana wa Mfalme wa Uingereza likiwasili ksatika mitaa ya Mji Mkongwe.
MWANA wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles akisalimiana na Vijana wa Scout.
MWANA wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles,akisalimiana na Kiongozi wa Scout katika mitaa yac Mji Mkongwe.
MTEMBEZA Watalii akitowa maelezo kwa Mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles, alipotembelea Mji Mkongwe wakati wa ziara yake Zanzibar.
WANANCHI wakimlaki Mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles alipotembelea Mji Mkongwe wa Zanzibar.
MWANA wa Mfalme wa Uingereza akitembelea maduka ya bidhaa za Kitalii za Vinyongo katika mitaa ya Shangani.
MKE wa Prince Charles Camilla akiwasalimu Wananchi katika Mji Mkongwe wa Zanzibar alipokuwa na ziara ya siku moja Zanzibar.
MWANA wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimuaga Mgeni wake Prince Charles, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Zanzibar.
ni upuzi mtupu huyo mtoto wa mfalme alikuwa apewa sheha swaleh maviyambuzi amtembeze jee kwani akija mtoto wa mfalme jemshid watamtembeza
ReplyDelete