Habari za Punde

MWANAMME ALIYEJIFANYA JIKE KWA KUVAA BUIBUI MIKONONI MWA POLISI

Na Mwantanga Ame

POLISI mjini hapa inaendelea kumshikilia kijana mmoja wa kiume aliekamatwa bandarini wiki iliyopita akiwa amevalia nguo za kike likiwemo buibui.

Mwanamme huyo, Ali Khamis Hamad alibambwa na polisi muda mfupi kabla ya kutaka kupanda boti kuelekea Dar es Salaam na baada ya kupekuliwa alikutwa na vitu mbali mbali vinavyoashiria kuwa yeye ni mwanamke.


Kwa mujibu wa Polisi, Hamad alikutwa amevaa baibui huku akiwa amevaa sidiria na kujiwekea machungwa kifuani kwake kwa lengo la kujifananisha na mwanamke.

Tukio la kukamatwa kwa kijana huyo lilitoa hisia tofauti kutoka kwa wananchi ambao haraka walimkabidhi kwa polisi kwa uchunguzi zaidi.

Mtu huyo alikuwa akishikiliwa na polisi Madema kwa uchunguzi.

Hata hivyo, habari za kuaminika zimeeleza kijana huyo aliefahamika kwa jina la Ali Khamis Hamad, baada ya kufanyiwa uchunguzi alibainika kuwa ni mwenyeji wa Bagamoyo na kwamba alikuja Zanzibar baada ya kuitoroka familia yake na alipoamua kurudi kwao ndipo alipojifanya kuwa mwanamke.

Habari ambazo hazikuthibitishwa zinadai kuwa Hamad kabla ya kwenda Zazibar, ndani ya familia yake alianza kuonekana akifanya mambo ya ajabu ajabu baada ya kurudi masomoni Mzumbe, Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mjini Magharibi, Azizi Juma alithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo akiwa katika mazingia hayo, lakini alisema hataweza kuzungumzia tukio hilo kwa vile linachunguzwa na Makao Makuu ya polisi. Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.