Habari za Punde

Azam Bingwa Mapinduzi Cup 2012, Mshindi wa Pili Jamhuri.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi Kombe la Ubingwa Mapinduzi Cup Nahodha wa timu ya Azam Agrey Moris.  
 Wachezaji wa timu ya Azam wakishangilia Ubingwa wao baada ya kukabidhiwa Kombe lao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, uwanja wa Amaan baada ya kuifunga timu ya Jamuhuri kwa 3-1
Washindi wa Pili wa Kombe la Mapinduzi timu ya Jamuhuri wakivishwa nishani na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baolizi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Jamuhuri kabla ya kuaza kwa mchezowa Fainali na timu ya Azam.imeshinda 3-1 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Azam kabla ya kuanza kwa mchezo wa Fainali na timu ya Jamuhuri,Azam imeshinda 3-1

 Wachezaji wa timu ya Azam wakiwasalimia Wachezaji wa timu ya Jamuhuri kabla ya kuanza cha mchezo wa Fainali timu ya Azam imeshinda 3-1, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan. 
 Kikosi cha timu ya Azam kilichotowa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 12-1-2012, uwanja wa Amaan.
 Washindi wa Pili wa Kombe la Mapinduzi timu ya Jamuhuri ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuuza kwa mchezo wao wa Fainali na Azam.
 Hivi ndivyo ilivyoluwa wakati wa mchezo wa Fainali kulikuwa na visa vya hapa na pale na kurushwa kwa njiwa huyu uwanjani hatimae kuagukia upande wa jukwaa la orbits.


Mshambuliaji wa timu ya Azam Kipre Tchetche, akimpita beki wa timu ya Jamuhuri Juma Omar, wakati wa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi, timu ya Azam imeshinda 3-1. 
 Mshambuliaji wa timu ya Azam John Bocco , akimpita beki wa timu ya Jamuhuri Salim Suleiman,  

 Wapenzi wa mchezo wa Soka Zanzibar wakifuatilia mchezo wa Fainali kati ya timu ya Jamuhuri na Azam uliofanyika uwanja wa Amaan.
 Beki wa timu ya Azam Agrey Moris, (kulia) akimzuwai mshambuliaji wa timu ya Jamuhuri Bakari Khamis.katika mchezo wa fainali, timu ya Azam imeshinda 3-1.  
Shabiki wa timu ya Azam akisherehekea Ubingwa wa timu yake huku akiwa amevua suruali na kubaki na nguo ya ndani uwanjani hapo, ikiwa ni kinyume na desturi na silka za Mzanzibar.    
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi mwandishi wa habari bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi Ali Bakari (Cheupe) kikombe na fedha taslimu shilingi laki moja.  
Wapenzi wa timu ya Azam wakishangilia timu yao baada ya kumalizika kwa mchezo wa Fainali uwanja wa Amaan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.