Habari za Punde

Uzinduzi wa Soko la Jumapili (Sunday Market) Michenzani Kisonge.`

 Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar, ambao ni Wadhamini wa Ufunguzi wa Soko la Jumapili Michezani nao wakitowa huduma ya ushauri  wa ufunguzi wa Akauti ya Akiba.   
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Seif Ali Iddi, akitowa nasaha zake katika Ufunguzi wa Soko la Jumapili katika viwanja vya Kisonge Michezani.  
 Waziri wa Wizara ya Uwezashaji Kiuchumi Mhe.Haroun Ali Sulaiman, akitowa maelezo ya uazishwaji wa soko hilo litakuwa kila jumapili katika Viwanja hivyo. 
 Wajasiriamali wakiwa katika meza zao wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akitowa nasaha zake na kuzinduwa Soko hilo. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akipata maelezo ya moja ya bidhaa za wajasiriamali alipotembelea mabanda hayo baada ya kuzinduwa soko hilo.    
 Wafanyakazi wa KCB, Tawi la Zanzibar wakitowa maelezo kwa Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, huduma wanazotowa kuwawezesha Wananchi kupata Mkopo wa Kujengewa Nyumba za Kisasa. huduma hiyo inapatikana katika Benki hiyo.   
Wajasiriamali Wafakifanya biashara katika viwanja vya Kisonge Michezani baada ya kufunguliwa soko la Jumapili.  
 Wajasiriamali wakitowa huduma ya kwa Wananchi waliofika katika Soko la Jumapili Michezani, banda hili linauza Uji wa Ngano na Vyakula vikavu.  
Wananchi waliohudhuria katika Ufunguzi wa Soko la Jumapili wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  akiwahutubia. 





Watoto kutoka kijiji cha Kiongoni Makunduchi wakicheza ngoma ya Kiaso, katika sherehe za uzinduzi wa Soko la Jumapili Michezani Kisonge.  

1 comment:

  1. ASALAMU ALAYKUM.
    HIO SIO SUNDAY MARKET KWA TUNAYOONA KWENYE HIO PICHA ,BALI NI HIGH STREET MARKET HIO, NA HAO VIONGOZI WANAJUA KABISA.LAKINI BASI TUUUUU.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.