Habari za Punde

ZANAIR Kuiwezesha Swahili Centre Kuongeza Ushiriki wa Pemba Katika Tamasha la Busara

Kutoka Kushoto-Mwale,Violet Maila, Ashish Nagewadia, Kheri,Rosie Carter na Mahsin Basalama

Kutoka Kushoto ni Solomon Mwale,Ashish Nagewadia  na Kheri Jumbe

Kampuni ya ndege ya ZANAIR imetoa ufadhili wa Shilingi milioni tatu (3) kwa kituo cha Swahili Center ili kuwawezesha kuongeza ushiriki wa Pemba katika Tamasha la Sauti za Busara linalotegemewa kufanyika Zanzibar kuanzia tarehe 8 hadi 12 Februari, 2012.

Akizungumza katika mkutano na Wanahabari katika jengo la kampuni hiyo liliopo Migombani-Unguja, Meneja Mauzi na Masoko wa kampuni Bw. Ashish Nagewadia alisema “ Ni faraja kubwa kwetu kupata fursa ya kuvifadhili vikundi vya Mkota na Juhudi kutoka Pemba. 

ZanAir imekuwa ikifanya safari za kwenda na kutoka Pemba tangu 1999 kwa mafanikio makubwa kutokana na mashirikiano ya wakaazi wa Pemba - sasa tuna safari tatu kwa siku. Kupitia ufadhili huu, tunapenda kutoa SHUKRANI ZA DHATI kwa wakaazi wote wa Pemba.”


Aidha, Bw. Nagewadia alisema kuwa ufadhali wa tukio hilo ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 20 toka kampuni hiyo ianze kutoa huduma za safari za ndege hapa Zanzibar mwaka wa 1992.

Kwa upande wa Swahili Center, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Bw. Kheri Jumbe alisema kuwa dhamira ya kushirikiana na ZanAir katika kuongeza ushiriki wa vikundi vya sanaa kutoka Pemba katika Busara na kumelenga kuvitangaza kimataifa kwa lengo la kuvitafutia ajira stahili na endelevu.

“Kwa mtazamo wetu, Pemba kuna vikundi vya sanaa za maoenesho za asili vyenye uwezo na wa kutoka kukubalika hata kimataifa. Ukosefu iliopo unaosababisha vikundi hivyo kubaki katika hali duni ni kutopewa fursa ya kuonekana katika majukwaa ya kimataifa kama vile Busara. Hivyo tunawashukuru ZanAir kwa kuwezesha kulitimiza lengo letu kwa mara hii,” alisema Mkurugenzi wa Swahili Center.

Akitoa maelezo kuhusu vikundi vitavyoshiriki kupitia ufadhili huo, Mkurugenzi wa Sanaa wa Swahili Center Bw. Mahsin Basalama alivitaja vikundi vya Mkota Spirit Dancers (Mkoani) and Juhudi Taarab (Chake-Chake) kuwa ndivyo vilivyo chaguliwa kushiriki tamasha la Busara mwaka huu.

“Vikundi vya Mkota na Juhudi ni katika vikundi vilivyo onesha uwezo wa hali ya juu katika mradi wetu wa 100% Zanzibari na ndiyo sababu ya kuvipendekeza kutumbiza katika Tamasha la Busara, “ alisema Basalama.

Katika kutoa maelezo zaidi, Basalama aliongeza kuwa mtunzi na mwimbaji maarufu wa kutoka Pemba, msanii Ali Said ‘Wazera’ atajumuika na kundi la Juhudi katika onesho lao kwa kuwaletea wapenzi wa Taarab asilia nyimbo zake maarufu kama vile ‘Bora Niombe’ na ‘Karamu’.

Ufadhili wa kutoka ZanAir utatumika katika kugharamia usafiri wa vikundi hivyo viwili pamoja na malipo yao ya kisanii, posho za kutwa, malazi na usafiri wa ndani wakiwa Unguja.

Kituo cha Swahili Center ni taasisi isiyo ya kiserikali (NGO ya kujitegemea) kilichoanzishwa kwa dhamira ya ‘kuchangia maendeleo ya sanaa za maonesho asili zitokazo hapa Zanzibar na mwambao wa waSwahili (Kenya, Tanzania Bara, Comoro nk) kupitia uwezeshaji wasanii, uwasilishwaji wa kazi za sanaa kwa jamii, ubunifu wa kazi za sanaa mpya pamoja na usambazaji kwa walengwa walio nje ya mijini.’

Kwa maelezo zaidi kuhusu taarifa hii, tafadhali wasiliana nasi kupitia anwani zifuatazo: -


ZanAir Ltd.

Ashish Nagewadia
Sales, Reservations & Marketing Manager
E: ashish@zanair.com


Swahili Performing Arts Center

Kheri A.Y. Jumbe
Managing Director
E: kheiri.jumbe@swahili-center.org
Mobile: 077.362-0202

1 comment:

  1. Ahsante sana Ndugu Othman, blog yako bomba sana..Unajitahidi sana..Nakuomba utusaidie kuwa Tamasha linaitwa Sauti Za Busara..Nafahamu kuwa wakati wa uandishi, wengi tunakamata neno la Busara na Sauti tunalisahau....hata wazungu nao, " are you going to Busara festival" ? Ahsante Sana..Mungu akuzidishie..Nawapongeza Kheri na Mahsin bila kumsahau Ashish wa Zanair....
    Simai

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.