Habari za Punde

Dk Shein Ahudhuria Maziko ya Mwakilishi Salum Amour Mtondoo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kushoto)akijumuika na Viongozi na Waislamu wengine kumswalia Marehemu Salum Amour Mtondoo,aliyekuwa Mwakilishi wa CCM Jimbo la Bububu Mkoa Mjini Magharibi Unguja, katika msikiti wa Ijumaa Bububu ,Marehemu alizikwa jana Kijijini kwao Bumbwini Kaskazini B
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziAlhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akijumuika na Viongozi na Waislamu wengine katika mazishi ya aliyekuwa Mwakilishi wa CCM Jimbo la Bububu Mkoa Mjini Magharibi Unguja,Marehemu Salum Amour Mtondoo,aliyezikwa jana Kijijini kwao Bumbwini Kaskazini B.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Salum Amour Mtondoo, aliyekuwa Mwakilishi wa CCM Jimbo la Bububu Mkoa Mjini
Magharibi Unguja,huko kijijini kwao Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B.

Picha na Ramadhan Othman IKULU

1 comment:

  1. Jamani wapi tunaelekea mnaweka bendera ya ccm!! muogopeni ALLAH mimi ningeomba kila kiongozi aliye serikalini aweke usia akifa jeneza lake lifunikwe na kitambaa chenye maneno matukufu ya LAILAHA ILLA LLAH MUHAMMAD RASUL LLAH. Kwani huko tuendako hutoulizwa mambo ya ccm wala cuf. kwa hiyo hayo mabendera hayatokufaa kitu huko akhera.!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.