Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wafanyakazi wa Wuizara ya Habari na Taasisi zake baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Idara hizo leo, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa salama bwawani. kushoto Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdillah Jihad Hassan na Naibu wa Wizara hiyo Bihindi Hamad.
Baadhi ya Viongozi wa Idara mbalimbali za Wizara ya Habari Utamaduni,Utalii na Michezo wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais akihutubia katika Mkutano huo Ukumbi wa Salama Bwawani.
Viongozi wa Idara za Wazira hiyo na Wafanyakazi wakimsikiliza Makamu wa Kwanza Maali Seif Shariff, akitolea maelezo ya ziara yake kwa Wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kumaliza ziara yake leo katika Idara za Utalii.
Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar, akizungumzia kusahauliwa kwa Wafanyakazi wa zamani ambao wako katika muda wa kustafu kazi, wakati wa kuongezea mishahara wao wamesahauli ikiwa muda wao umebaki mchache, akieleza wakati wa Mkutano na M,akamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, katika ukumbi wa salama bwawani. 
Msanii Othman Makombora, ameitaka Wizara kuwapatia sehemu ya kufanyika shughuli yao ya sanaa sehemu waluoko ni vinyu na katika Jengo la Ngome kongwe.na kutaka serekali kuchukuwa hatua ya makusudi kuwaendeleza Vijana katika hii sanaa wakati Wazee tayari wengi wao wameshastaafu ikizingatiwa utamaduni utapotea na kutafuta wataalam kuja kutufundisha.
Mfanyakazi wa Kamisheni ya Utalii ameimba Serekali kuwapatia sehemu muafaka katika bandari na Uwanja wa Ndege kutowa huduma hiyo, ambayo ni moja ya sekta ya kuipatia mapato serikali na kukuza uchumi wa nchi kupitia Utalii.
Mfanyakazi wa Chuo cha Utalii Maruhubi ameiomba Wizara na Serikali kuunda Tume ya kuchunguza hali ya Mmomonyoko wa ardhi katika eneo la Chuo hicho kwa maana linazidi kuliwa na maji ya bahari.
Mfanyakazi wa ZBC redio Said Suleimn,amesema sasa tunatoka katika mfumu wa teknolojia ya Analogi na kuigia katika teknolojia ya Digitali na wafanyakazi waendane na mfumo huo Digitali kwa kupata mafunzo yanayoendana na hali hiyo na kuita wizara kuipatia usafiri wa uhakika katika shughuli zao za kila siku za habari.ili kuielemisha jamii katika sekta ya kupata habari mbalimbali.
Msanii wa sanaa ya Taraab Bi Fatma Issa,nae hakuwa nyuma katika maombo ya sanaa ya Taarab, amesema yeye anashindwa sehemu ya kurikodia nyimbo zake ili ziweze kumpatia chochote wakati wa kustaafu kwake.
Mfanyakazi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, ameiomba serikali kukifufu kituo chake cjha habari za utalii ili watalii wanapomaliza kutambela sehemu za historia na kutowa maelezo yake katika kituo hicho na kutowa taarifa ya wageni wakiwa nje ya nchi wanaotaka kuja kutembelea Zanzibar, hapo zamani kituo hicho kilikuweko darajani.
Mfanyakazi wa ZBC Nassra Nossor, akichangia kituo cha ZBC Tv kiwezeshwe katika mipango yake ya kutegenezea program mbalimbali za vipindi kwa wafanyakazi wake Tv ni kioo cha Jamii, na kutowa elimu.
Mwalim wa Chuo cha Utalii Maruhubi ameitaka Wizara kuchukuwa juhudi za makusudi katika ufanyaji wa majaribio katika mahoteli ufanywe na chuo hicho kuepusha upendeleo unaofanya na baadhi ya mahoteli kwa kuwaajiri wageni katikamahoteli hayo.
Mkurugenzi Mipango naSera Joseph Kilangi, akitowa maelezo ya baadhi ya michango ya Wafanyakazi wa Wizara Habari Utamaduni Utalii na Michezo, wakatika wa mkutano na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika ukumbi wa salama bwawani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akijibu baadhi ya michango ya Wafanyakazi wa Wizara ya Habari katika Mkutano wake na Wafanyakazi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Salamsa Bwawani, na kuhaidi kuyafanyika kazi michango yao hiyo.
Wafanyakazi wa Wizara ya Habari wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais akizungumza na Wafanyakazi baada ya kuwasikiliza baadhi ya Wafanyakazi waliotowa michango yao kwa Idara zao jinsi ya utendaji wa kazi.
No comments:
Post a Comment