Habari za Punde

Ofisi ya Vitambulisho Zanzibar yapata tena Vyeti vya Ubora wa Utengenezaji Vitambulisho Kimataifa.



 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Salum Maulid, akiwa na kimoja ya Vyeti vya Ubora wa Kimataifa vya Utengenezaji Vitambulisho,kulia Lead Auditor, Quality&Certification Division Avraham Rost, Mkurugenzi wa Vitambulisho Zanzibar Mohammed Juma Ame,Securty &Quality Consultant Securitree Inter. Ltd Israel, Merav Vered.
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Ikulu Salum Maulid, akizungumza katika sherehe za kukabidhi Vyeti vya Ubora wa Kimataifa wa Utengenezaji Vitambuliza, zilizofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
Mkurugenzi wa Vitambulisho Zanzibar Mohammed Juma Ame, akitowa maelezo ya mafanikio yao ya kushida katika kiwango cha Kimataifa cha Utengenezaji wa Vitambulisho, wakati wa sherehe za kutunukiwa Vyeti hivyo iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
Wazee wa meza kuu wakimsikiliza Avraham Rost, Lead Auditor Quality&Certification Division, akizungumza katika sherehe hizo za kukabidhi Vyeti vya Ubora wa Kimataifa vya Utengenezaji Vitambulisho, kwa Ofisi ya Vitambulisho Zanzibar 
Mameneja wa Ofisi ya Vitambulisho Zanzibar wakiwa makini wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Salum Maulid, akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wa Ofisi hiyo.
Wafanyakazi Ofisi ya Vitambulisho wakiwa makini kusubiri kupoke Vyeti vyao vya Ubora wa Utengenezaji Vitambulishi Kimataifa, kwa kazi inzuri wanayofanya kuboresha utegenezaji wa Vitambuli hivyo hapa Zanizbar na kutowa huduma hiyo kwa Taasisi mbalimba. 


Mkurugenzi wa Vitambulisho Zanzibar Mohammed Juma Ame, akizungumza na waandishi wa habari mafanikio ya Osifi yake kufanya vizuri katika utegenezaji wa Vitambulisho na kupata Ubora wa Kimataifa kwa miaka sita sasa.   
Mkuregenzi wa Vitambulisho akiwa katika picha ya pamoja na Mameneja Wataalam kutoka Israel, waliofanya uchunguzi wa ubora wa vitambulisho vinavyotengenezwa katika Ofisi yake.
Jopo la Wafanyakazi wa Ofisi ya Vitambulisho wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na Vyeti vyao baada ya kukabidhiwa, sherehe hizo zimefanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.

5 comments:

  1. Congratulations to the office of identity cards to get such certification, we have no worries with technology but the problem lies in the ethics behind, because technology without ethics is useless, we want to see technology help all Zanzibaris not technology that marginalize some and favor others.We need to see those complaints of deprivation identity cards. The second thing is we also want to see identity cards to be integrated with information systems from other stakeholders like birth and death registration office, Its is even better to be integrated with ministry of education and health to capture student who sit for an exams. It can also be used even for shopping, I remember I have visited one of the Asian countries I went to the store, because my face look like them shopkeeper gave me a price and later asked me if I have ID the price will be reduced by seventy percent.

    ReplyDelete
  2. Wacheni kuhadaliwa na wana wa Israel, kila siku wanakupongezi nyinyi tuu kwa vitambulisho vizuri. Wana lao hao wanalitafuta.

    ReplyDelete
  3. sasa munafkiri hao waisrael wao ndio ambao walipewa hiyo tenda, na sasa wanajisifu wenyewe, hicho ni kiini macho.

    ReplyDelete
  4. Anony wa pili umenena. Ama hili la vitambulisho naona kama tumeenda mrama hasa kwa kutegemea misaada. Maana mradi huu ulifahdhiliwa asilimia mia na Mmarekani na tenda ya kutengeneza ikaenda kwa Myahudi. Upo hapo?

    Hivi sasa Data zote za Wazanzibari wanazo waheshimiwa kwenye Super Computers zao. Wenzetu wakifanya miradi nyeti kama hii husomesha wazalendo wao kwanza na kuwapa uwezo si kutegemea ufadhili.

    ReplyDelete
  5. Nakubaliana na wewe anonym wa mwisho: Nakumbuka wakati wanatekeleza huo mradi walipita ofisi zote za serikali na kuchukuwa sensitive information za computer ambazo zilikuweko ikiwepo MAC address sasa mimi nna uhakika wanaaccess ya computer karibu zote za serikali na data zote ambazo tunahifadhi humo, pia nilikuwa nashangaa kuna uhusiano gani wa kutengeneza vitambulisho na data zilizokuwemo kwenye computer mawizarani

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.