ASSALAAMU 'ALAYKUM WARAHMATUL LLAAHI WABARAAKATUH.
JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KIISLAM WA CHUO KIKUU CHA MUHIMBILI (MSAMU)
2011 - 2012
UTAMBULISHO;
Amma baada ya kumshukuru Allah (s.w) na kumtakia Rehma na Amani mtume wetu na mjumbe wake Muhammad (s.a.w) sisi ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Afya na utafiti wa tiba cha MUHIMBILI (Dar-es-salaam) tukishirikiana na vyuo vingine .
Tunapenda kuchukua nafasi hii ya kuandika hii nakala kwa ajili ya kuwafikishia ndugu zetu wa chini yetu (form one hadi form six). Sisi kama wanafunzi /waislam tulio katika elimu ya juu ya chuo tumeona kuwa tuna dhimma ya kuwasaidia ndugu zetu waliokatika kiwango cha chini cha elimu ambao tunahisi kuwa yanaweza kuwasaidia/kuwa na umuhimu katika masuala yao mazima ya kielimu.
Katika nakala hii tumeamua kiugawa katika vipengele vinne, ambavyo ni;
1. Namna ya kuiendea mtihani katika maandalizi yote ya kivitendo na kiimani
2. Namna gani utayapokea matokeo yako kwa namna yoyote ile yatavyokuwa mazuri, mabaya au ya kati nakati
3. Namna ya kujiunga katika vyuo vikuu hususani kwa chuo cha afya Muhimbili na vinginevyo(katika suala zima la kiafya)
4. Hitimisho na ushauri
1 ;
MAANDALIZI YA MITIHANI
Katika kipengele hiki cha maandalizi ya mitihani na namna na yakujiandaa kuuelekea mtihani tumekigawa katika vipengele vikuu vinne kama ifuatavyo;
a. maana ya mitihani.
Mtihani ni kipimo cha imani (kidini), uelewa au ufahamu wa mtu juu ya kitu fulani kwa mfano Mwenyezimungu (s.w) ametuandalia mitihani mbali mbali kama maradhi au vifo ili kutupima imani zetu kama tutafaulu au tutafeli. Pia katika mashule yetu imeandaliwa mitihani ili kutupima ufahamu uelewa wetu juu ya yale ambayo tunayasomea.
b. Namna ya kujiandaa na mitihani
Katika namna ya kujiandaa na mitihani tumeamua kugawa katika namna kuumbili;
(i) Maandalizi ya kivitendo
Katika maandalizi ya kivitendo mtu hujiandaa pale tu anapoingia katika shule kutokana na kufahamu kuwa ipo siku atafanya mitihani na kumaliza shule. Mitihani hiyo ndiyo ambayo itakufanya uweze kufaulu na kwenda katika ngazi ya juu zaidi au kutokwenda.
Hivyo basi hatuna budi kujiandaa kwa namna yoyote ile iwayo ili tuweze kufaulu na kuweza kuendelea katika ngazi za juu zaidi na hatimaye kuweza kutimiza yale malengo yetu.
(ii) Maandalizi ya kiimani.
Katika maandalizi haya mtu huanza katika ngazi ya kifamilia, kuanzia pale unapozaliwa hadi kufikia kiwango cha kuweza kujitegemea kwa maisha yako na hatimaye kuwa baba au kuwa mama.
Hivyo hatuna budi basi kuamini kuwa mitihani nikipimo cha kuamini Qadar (kheri au shari ) zinatokana na Mwenyezimungu (s.w). Hivyo basi hatuna budi kuelewa kuwa tunadhimma ya kutekeleza yale yote ambayo ndiyo sababu ya sisi kufaulu au kufeli katika mitihani hiyo (KIIMANI)
Hivyo katika maandalizi haya hatuna budi kuiendea mitihani yetu katika namna ambayo Mwenyezimungu (sw) ataipendelea ambayo ni;
i. kusimama visimamo vya usiku,
ii. Kuingia katika chumba cha mtihani haliyakuwa tumetia udhu,
iii. Kuwahi katika eneo la tukio (chumba cha mtihani) ili kuyazoea mazingira ya eneo husika,
iv. Kumtanguliza Mwenyezimungu kwa kusoma suratul fat-ha(quran 1) na suratul muadhwatain (falaq& nnasi) mwisho ni saratul ikhlas ni vizuri idadi ya witri ikiwezekana.
v. Kumsabahi Mwenyezimungu kwa nyiradi mbalimbali (fupifupi).
iii. namna ya kujibu mtihani
Katika kujibu mtihani mambo ya msingi ya kuzingatia ni kama ifuatavyo;
a) Kuanza na swali unalolijua ambalo pia ni lenye alama nyingi(marks)
b) Kutumia uwezo wako wote katika kulijibu swali ambalo unalijua
c) Kwa swali ambalo huna uelewa nalo kabisa ni vizuri usilifanye na uliache kwani utapolifanya utaonyesha udhaifu wako kwa wasahilishaji au ulifanye mwisho baada ya maswali yote unayoyafahamu kuyafanya.
d) Ni vizuri kufanya maswali yote kama unayaweza na muda upo mfano mtihani wenye maswali kumi na mbili 12 basi fanya yote kumi na mbili
e) Ni vizuri pia kuwa makini na muda wa kufanya mtihani kwani muda ni s ehemu pia katika mtihani
2.
NAMNA YA KUYAPOKEA MATOKEO YETU
Matokea
ni zao au chumo ambalo hutokea baada ya kufanyika kwa jambo fulani ,hivyo
machumo yaweza kuwa ni kuridhisha au kutoridhisha. Hivyo matokeo ya mitihani
yetu yaweza kuwa ni mazuri , ya kati na kati au yasiokuwa mazuri.
i.
MATOKEO MAZURI;
Hayo
ni matokeo ambayo mtu huyapata yakamuwezesha yeye/wewe kwenda katika ngazi ya
juu ambayo anaitarajia/ unatarajia.
Watu
wengi wapatapo matokeo mazuri hupata kiwewe kutokana na furaha waliyonayo na
kukurupuka na kushindwa kufanya uamuzi uliosahihi.La umuhimu nikumuomba
Mwenyezimungu na kumshukuru na kutafuta ushauri kwa wale walio juu yako ni lipi
la kufanya kabla ya kufanya uwamuzi.
ii.
KATI NA KATI
Haya
ni matokeo ambayo mtu hupata alama/matokeo mazuri lakini kutokana na alama hizo
hazikumuwezesha yeye kupata kuisoma kozi ambayo ameitarajia. Mfano mtu ambaye
amepata gredi ya tatu (Division iii) na ametaka asome udaktari (medicine). Muhimbili
. Ni ngumu kupata kozi hiyo lakini kuna baadhi ya vyuo ambavyo anaweza kupata
chuo kutokana na alama hizo. Hivyo basi ni uzuri kutafuta ushauri kupitia
wanafunzi/waislam walio vyuoni ili kuweza kumshauri cha kufanya.
iii.
MABAYA (YASIYORIDHISHA)
Haya
ni matokeo ambayo hayatamuezesha mtu kujiunga, kuingia elimu ya juu (vyuo)
katika kiwango cha shaada(degree) maranyingi watu hawa huwa ni wenye kukata
tamaa na wengine kuamua kurudia mtihani ili waweze kufaulu hali yakuwa kuna
njia nyingine (mbadala) ambazo wanaweza kupitia na kufikia malengo yao mfano
ASTASHAHADA (CERTIFICATE), STASHAHADA (DIPLOMA), na hatimae kufikia SHAHADA
(DEGREE) na kisha kuendelea ngazi au kiwango cha juu zaidi kielimu.
USHAURI.
Tusingependa kumshauri mtu arudie
mtihani kwa maana utafiti umeonyesha kuwa wengi wanaorudia mtihani hawafanyi
vizuri,Hivyo ndo maana tumetoa nakala hii kuonyesha kuwa njia mbadala ambayo ni
zaidi ya kwenda kusomea ualimu.
Lakini kwa wenye kuamua mitihani
yawapasa wafanye yafuatayo kwanza:
1. Kufanya tathmini ya kina sababu
zilizopelekea matokeo yake kuwa hivyo
2. Je sababu hizo zinatatulika kirahisi
3. Basi atatue matatizo hayo ndio aweze
kurudia mtihani
Miongoni mwa sababu zinaweza kuwa;
a) Sababu za ndani/binafsi (internal
factor)
b) Sababu za nje (external factors)
Sababu zote hizi mwisho wa siku huchangia katika kuleta matokeo ama
mazuri au mabaya, zinaweza kuwa za kiuchumi, kifamilia, kimazingira, kijamii au
kitaasisi (shule).
Baada ya kutatua hizo sababu tunaweza kukubaliana na wewe katika mawazo
yako ya kurudia mtihani wako.
Tumezikusanya hivi baadhi ya shule
na vyuo kulingana na michepuo inayopatikana katika vyuo hivyo ili ujue ni vyuo
gani unaweza kuvichagua.
SOME
OF THE FACULTIES WITH THEIR RELATED
UNIVERSITIES
AND COLLEGES.
-ALLIED
HEALTH SCIENCE;
I. Hubert Kairuki Memorial University (HKMU)
HK University Private Dar es Salaam
II. International Medical and Technological
University (IMTU) IM University Private Dar es Salaam
III. Kilimanjaro Christian Medical College
(KCMC) KC University College Private Kilimanjaro
IV. Muhimbili University of Health and Allied
Sciences (MUHAS) MH University Public Dar es Salaam
V. Weill Bugando University College of Health
Sciences (WBUCHS) BU University College Private Mwanza.
VI. All universities under Ministry of health
-BUSINESS;
i. College of Business Education (CBE) Dodoma
CBD Non-university Public Dodoma
ii. .College of Business Education (CBE) DSM
CB Non-university Public Dar es salaam
iii. Institute of Accountancy Arusha (IAA) IA
Non-university Public Arusha.
iv. Institute of Finance Management (IFM) IF
Non-university Public Dar es Salaam
v. Mkwawa University College of Education
(MUCE) UDM University College Public Iringa
vi. Moshi University College of Cooperative
and Business Studies (MUCCOBS) MC University College Public Moshi
vii. Mzumbe University (MU) MU University
Public Morogoro
viii. Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
TA Non University Public Dar es Salaam
ix. Zanzibar Institute of Financial
Administration (ZIFA) ZF Non-university Public Chwaka Zanzibar.
-ENGINEERING;
i. Ardhi University (ARU) AR University Public
Dar es Salaam
ii. Dar es Salaam Institute of Technology
(DIT) DT Non-university Public Dar es Salaam
iii. Mbeya Institute of Science and Technology
(MIST) MB Non-university Public Mbeya
iv. Sokoine University of
Agriculture (SUA) SU University Public Morogoro
v. St. Joseph College of Engineering &
Technology (SJCET) JD Non University Private Dar es Salaam
vi. St. Joseph Institute of Information
Technology (SJIIT) JS Non University Private Songea
-ARTS
i. Community Development Training Institute
Tengeru (CDTI) CD Non-university Public Arusha
ii. Institute of Social Work (ISW) SW
Non-university Public Dar es Salaam
iii. Open University of Tanzania (OUT) OU University
Public Dar es Salaam
-EDUCATION;
i. Dar es Salaam University College of
Education (DUCE) UDD University College Public Dar es Salaam
ii. Mwenge University College of Education
(MWUCE) MW University College Private Moshi
iii. Sebastian Kolowa University College
(SEKUCO) SK University College Private Tanga
iv. St Augustine University of Tanzania
(Mtwara Centre) (SAUT) SAM University Center Private Mtwara
v. St Augustine University of Tanzania (SAUT)
SA University Private Mwanza Tanzania Commission for Universities
vi. State University of Zanzibar (SUZA) SZ
University Public Zanzibar
-MORE
FACULTIES;
i. St John’s University of Tanzania (SJUT) SJ
University Private Dodoma
ii. Institute of Rural Development Planning
(IRDP) RD Non-university Public Dodoma
iii. Iringa University College (IUCO) IU
University College Private Iringa
iv. Kampala International University Dar es
Salaam Center (KIU) KU University Private Dar es Salaam
v. Makumira University College (MUCO) MK
University College Private Arusha
vi. Mount Meru University (MMU) MM University
Private Arusha
vii. Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA)
MN Non-university Public Dar es Salaam
viii. Ruaha University College (RUCO) RU
University College Private Iringa
ix. St John’s University of Tanzania (SJUT)
(Msalato Centre) SJM University Centre Private Dodoma
x. St John’s University of Tanzania (SJUT) (St
Mark Centre) SJD University Centre Private Dar es Salaam
xi. Stefano Moshi Memorial University College
(SMMUCO) SM University College Private Moshi
xii. Teofilo Kisanji University (TEKU) TK
University Private Mbeya
xiii. Tumaini University Dar es Salaam College
(TUDARCO) TD University College Private Dar es Salaam
xiv. University of Arusha (UOA) UA University
Private Arusha.
xv. University of Dar es Salaam (UDSM) UD
University Public Dar es Salaam.
xvi. University of Dodoma (UDOM) DM University
Public Dodoma.
- Si hivyo tu ila pia kuna vyuo ambavyo
havikujiingiza katika sual la TCU kama chuo cha kiislam cha Morogoro
(MUM),………………………..
Pia kwa maelezo zaidi ni vizuri kuingia
katika website za vyuo vyenyewe (mfano MUHIMBILI UNIVERSITY) kwani kuna maelezo
ya kina zaidi ya haya na pia hata muda wa kozi, ada, lini fomu za kujiunga
zinatoka na tarehe ya kurudisha pia. Pia unaweza kuingia katika website ya TCU
wenyewe (www.tcu.go.tz) pia wanamaelezo kuhusuvigezo vya kujiunga na chuo, ada, muda wa
kujisajili, namna ya kujisajili, pia vitu vinavyohitajika nk.
3.
NAMNA YA KUJIUNGA KATIKA SECTA YA AFYA
-Katika
suala hili ambalo ndio wazo kuu la uandishi wa nakala hii, tumeongelea upande
wa afya hususani katika chuo chetu cha MUHIMBILI kuwa ndio waanzilishi wa suala
hili kwa ujumla. Sababu kuu ni kutokana
na udhalilishaji wa kijinsia ambao tunakutana nao katika mazingira yetu kikazi
kwani utu haupo, mfano: wanaume huweza kufanyiwa vipimo na wanawake pia kwa
baadhi ya sehemu wanawake hufanyiwa vipimo na wanaume.
Mifano hai ipo hususani kwa
kinadada zetu au hata mama zetu pindi wapatapo ujauzito na kuhitaji msaada wa
matibabu na ni madhila mangapi wanayoyakuta.Hivyo kutokana na hilo tumeonelea
ni bora sisi kama waislam tuna dhimma ya kulinusuru hilo.
Hili ni kama jambo fardhi (kifaya)
ambalo wachache wanaweza kufanya kwa ajili ya wengi, hivyo basi sisi hatuna
budi kusoma ili tuwasaidie ndugu zetu kutokana na hali/tatizo hili. Kama
ilivyoelezwa katika vipengele vilivyotangulia kuwa sio kupata matokeo mabaya
kwani ndio mwisho wa ndoto zetu bali tuwe na ufahamu kuwa ziko namna / njia
ambazo tunaweza kutumia ili tuweze kufikia malengo yetu.
Hivyo njia ambazo tunaweza
kuzitumia hatimaye tuweze kutumiza malengo yetu ni kwa kutumia kozi fupi za
awali kama diploma na hatimaye tukaweza kuzifikia ndoto zetu, kama wanaotaka
kuwa madaktari (specialist).
Hivyo mwisho kabisa tunaambatanisha
na nakala ambazo zinaelezea kozi, muda wake ,alama zinazohitajika , na kazi
ambayo wewe utaifanya kutokana na kozi hiyo ulivyo ichagua . Kuhusu gharama zinazohusiana na ADA , MALAZI
, CHAKULA< MATIBABU, na maelekezo mengine yanapatikana katika fomu ya
kujiunga na chuo.
Fomu zetu za kujiunga na chuo cha afya na tiba cha Muhimbili fomu zinapatikana
chuo au kupitia katika website ya Chuo (www.muhas .ac.tz).
THE
INSTITUTE OF ALLIED HEALTH SCIENCES IN A PUBLIC INSTITUTION FOR TRAINING
MIDDLE
LEVEL HEALTH CARE.
PROVIDERS
TANZANIAN LEADING TO AWARD OF DIPLOMA AND ADVANCED
DIPLOMA
IN VARIOUS ACADEMIC.
PROGRAMMES.
The Institute is in position to provide in
Tanzania learning, research and service in Allied Health Sciences that are
based on curative, preventive, rehabilitative and restorative health care.
8.1.1 Diploma in Medical Laboratory Sciences
This is a six-semester Diploma in Medical
Laboratory Sciences (DMLS) Programme. It intends to train health personnel
capable of managing medical laboratory and diagnostic services focusing on
preventive curative and rehabilitative health care. Students are also trained
to carry out research activities relevant to provision of quality health in laboratory
services.
8.1.1.1
Entry requirements
Direct Entry
Credits in Biology and Chemistry and one in either Physics or Mathematics at
‘O’ level.
Equivalent Qualifications
Laboratory Assistant with three years’
experience who has passed the selection examination recognized by the
University and must have ‘O’ level secondary school certificate.
8.1.2
Diploma in Environmental Health Sciences
This
is a six-semester Diploma in Environmental Health Sciences (DEHS) programme. It
is intended to enable Environmental Health graduates to organize, plan, manage,
supervise, monitor and evaluate, comprehensive preventive and promotional
health services targeted at individuals and communities at all levels of the
health care delivery system in the country and elsewhere.
This
program is also intended to ensure that EHOs are provided with state of the art
knowledge and skills, enabling them to be catalysts for sustainable and
innovative health solutions by communities.
8.1.2.1
Entry requirements
Direct Entry
Pass in English and three credit passes, one in Mathematics and two other out
of Physics, Chemistry and Biology at ‘O’ level.
Equivalent Qualifications
Health Assistant with three years experience who has passed the selection examination
recognized by the University and must have ‘O’ level secondary school
certificate.
8.1.3 Diploma in Diagnostic Radiography
This is a six-semester Diploma in Diagnostic Radiography (DDR) programme.
The aim of the programme is to train radiographers to be able to use different
kinds of X-rays CT IMRI ultrasound, CR and digital Radiography facilities scans
and to investigate diseases injuries in patients. They should also be able to
care for patients and maintain radiological facilities, i.e. Radiological and
Imaging facilities in their place of work. The radiographer will also be
trained to interpret plain radiographs and give intravenous injections where
applicable.
8.1.3.1 Entry Requirements
Direct Entry
C grade or higher passes in three out of Physics, Chemistry, Biology and
Mathematics and at least D grade pass in English. Physics is a major subject.
Equivalent Qualifications.
Radiographer Assistant with three years experience who has passed the selection
examination recognized by the University and must have ‘O’ - level secondary
school certificate.
8.1.4 Diploma in Orthopaedic Technology
This is a Six-Semester Diploma in Orthopaedic Technology (DOT) Programme.
The programme is intended to impart knowledge and skills to students on the
evaluations, design, and fitting of different orthopaedic appliances, equipment
and materials. It also aims to impart the correct attitude in students towards
patient care.
8.1.4.1 Entry requirements
Direct Entry
Three credit passes out of Physics, Chemistry, Biology or Mathematics at
O’level. Credit pass in engineering subjects is also acceptable as the third
credit pass. Equivalent Qualifications Candidates must have certificate in
lower limb Prosthetics or Orthotics and must have two credit passes in science
subjects at “O” level.
8.1.5 Diploma in Pharmaceutical
Sciences.
This is a Six Semester Diploma in Pharmaceutical Science (DPS) Programme. It is
intended to train competent Pharmaceutical technician who can manage a district
or a health care centre pharmacy under the supervision of a registered
pharmacist. The training mainly focuses on imparting knowledge and skills to
students on compounding and dispensing drugs to in-patient and out-patients in
the health facilities. Also students are trained on providing drug related
information to patients and the public at large.
8.1.5.1 Entry Requirement
Direct Entry
Three credit passes which must include Maths, Chemistry and English with a pass
in Biology and Physics.
Equivalent
Qualifications.
Pharmaceutical Assistant with three years
experience who has passed the selection examination recognized by the
University and must have ‘O’ level secondary school certificate.
8.1.6
Diploma in Nursing
The Diploma in Nursing is an integrated
training with midwifery and psychiatric nursing as options for which students
choose but all of them get the training in general nursing. The training is of
four academic years (8 semesters). Student’s progress is assessed by frequent
tests during the semesters and at the end of the academic year. Fifty percent
of the total marks is based on the results of the final examinations, the other
50% is from the continuous assessment tests.
8.1.6.1 Entry Requirements
i. Candidates
must have completed O-level education with a credit in Biology and two passes
in Chemistry and Mathematics or Physics.
ii.
Candidates must have completed secondary school education within three years
from the year of application.
8.1.7
Advanced Diploma in Nursing Education
This is a four-semester Advance Diploma in
Nursing Education (ADNE) Programme. The programme intends to produce nurse
teachers who will enhance the delivery of quality health education and health
care in the country.
8.1.7.1
Entry Requirements
Direct Entry: N/A
Equivalent Qualifications
Registered Nurse with two years experience, who has passed the matriculation
examination and must be a holder of ‘O’ level Certificate with credit/pass in
Chemistry, Biology and English.
8.1.8
Advanced Diploma in Dermatovenereology
This is a four Semester Advanced Diploma in
Dermato-Venereology (ADDV) Programme. Students are trained to diagnose and
competently manage most dermatological conditions, Leprosy, HIV/AIDS and other
Sexually Transmitted diseases (STDs) in the context of Primary Health Care
(PHC). The programme also intends to impart knowledge on how to plan and carry
out appropriate measures for prevention of Skin diseases and STDs. Students are
also trained to conduct operational research of both clinical and
epidemiological nature and apply the findings in the improvement of health
services in the community.
8.1.8.1 Entry Requirements
Direct Entry: N/A
Equivalent Qualification
Should have successfully completed any one of the following courses with an
overall good performance grade(s).
- Assistant Medical Officer (AMO) in Tanzania
In Other countries
- Medical Assistant
- Clinical Officer
- Nurse Clinician
- Family Nurse Practitioner Or an equivalent
level, AND must possess ‘O’ level secondary school certificate with passes in
Physics,Chemistry and Biology.
8.1.9 Advanced Diploma in Med. Lab.
Sciences
This is a four-semester Advanced Diploma in Medical Laboratory Sciences (ADMLS)
Programme.It intends to train health personnel capable of managing medical
laboratory and diagnostic services focusing on preventive curative and
rehabilitative health care. Students are also trained to carry out research
activities relevant to provision of quality health in laboratory services.
Direct Entry: N/A
Equivalent Qualifications
Medical Laboratory technicians who hold a good Diploma in Medical
Laboratory Sciences or its equivalent with two years working experience. Must
possess ‘O’ level Secondary School Certificate with passes in Physics,
Chemistry and Biology.
HITIMISHO;
Tunamshukuru
Mwenyezimungu (s.w) kwa kutuwezesha sisi kuweza kuiandika na kuiwakilisha kwa
wenzetu nakala hii ambao tunaona kuwa kuna umuhimu wa wao kuyajua mambo haya.
Pia kwa upande mwingine tunawashauri ndugu
zetu waislamu.Sisi ni katika wale wachache ambao tumechaguliwa na Mwenyezimungu
(s.w) kuweza kuiendea elimu hii ya sekula na ni wajibu kwetu kusoma kwa ajili
ya kuwanusuru waislamu wenzetu na uislamu kwa ujumla.
Hivyo ushauri sisi kama waislamu au wanafunzi
wenzenu ni ;
Tuwe wajumbe kwa wengine ambao wapo chini yetu
ili tuweze kuuinua uislamu na kuwanusuru waislamu wenzetu.
Tusibweteke (kujiamini) kwa yale machache
tunayoyajua.
Watu wajitahidi kufuatilia habari baada ya
kumaliza elimu zao. Hii ni ili kuweze kufikia katika kiwango cha juu zaidi
kielimu na kuweze kutimiza ndoto zetu.
Kwa mawazo, mchango, ushauri au lolote
wasiliana nasi kwa;
ABDALLAH ABDALLAH 0784-560 920
JUMANNE MASANJA 0716-322 839
MOHAMMED NYATI 0785820012
BAKARI MSONGAMWANJA 0717-963 033
SLIM 0713-624 903
BIWETE 0713-277 008
ALLY SAID assmohamm@hotmail or gmail.com
Angalizo:
piga simu kwa ajili ya kupata maelezo zaidi na
si kwa kusumbua watu kwani ni
wengi wanaosumbua na sisi ni wanafunzi pia
WABILLAHI
TAWFIIK.
safi sana ndugu zetu kwa ujumbe Mola awazidishie na ngoja tufatilie nasi ili tuangalie kama tutapata vyuo maana haya matokeo yanauma sana.
ReplyDelete