Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMATI ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shiriksho la Soka Tanzania (TFF), imeamuru mchezo kati ya Azam FC uliovunjika zikiwa zimesalia dakika chache, timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 wiki mbili zilizopita kwenye uwanja wa Azam, Chamazi urudiwe.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana jioni chini ya Mwenyekiti wake, Kamanda Mstaafu, Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, zimesema kwamba mchezo utarudiwa kwa sababu imebainika makosa yalikuwa ni ya waamuzi na si Mtibwa.
Kamati hiyo imebaini kuwa, waamuzi hawakufuata kanuni za kusubiri kwa dakika kumi, wakati wachezaji wa Mtibwa Sugar walipkuwa wamegomakabla ya kumalizika kwa mchezo.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa, Azam sasa itabaki na pointi 53 na mechi mbili, ikiwemo ile iliyotarajiwa kufunga pazia dhidi ya Kagera Sugar.
Uamuzi huo umekuja baada ya Mtibwa Sugar kukata rufaa ikipinga uamuzi wa kuipa ushindi Aam FC baada ya kuvunjika kwa mchezo wa awali.
Alipoulizwa namna alivyoupokea uamuzi huo, Katibu Mkuu wa klabu ya Azam FC Nassor Idrisa Mohammed, alisema hawana tatizo na hilo na kwamba watacheza mchezo uliopangwa kufanyika leo uwanja wa Chamazi.
No comments:
Post a Comment