Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dk Albina Chuwa amesema ufanisi mzuri kutoka kwa walimu wa makarani wa sensa, ni nafasi pekee ya kulinda hadhi na heshima ya Tanzania ya kuwa mfano wa kuigwa katika mataifa mengine Afrika kwa kufanya sensa yenye mafanikio.
Hayo ameyasema wakati wa mafunzo ya walimu wa wakufunzi wa makarani wa sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi wa Agosti mwaka huu ,katika ukumbi wa chuo cha mipango Dodoma.
Amesema lengo la Tanzania ni kufanya sensa yenye mafanikio kwa kupata takwimu sahihi zitakazo isaidia Serikali kupanga mipano ya maendeleo kama sensa nyengine zilizopita ambapo sensa ya mwaka huu ni sensa ya tano tangu kuanza kufanyika
Aidha amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini katika kupokea mafunzo hayo kwa vile wao ndio walimu watakao kwenda kuwafundisha wakufunzi wa makarani wa sensa, katika ngazi zote na kuhakikisha taarifa na takwimu sahihi zinapatikana.
Mafunzo hayo yatakayo chukua muda wa wiki mbili, yanawashirikisha washiriki wapatao mia moja na hamsini kutoka Tanzania nzima na yanalenga kuwapa elimu ya kuwafundisha wakufunzi wa makarani wa sensa katika ngazi za mikoa.
No comments:
Post a Comment