Na
Oscar Samba, AJTC
WAKAAZI
wa Muyuni wilaya ya Kusini Unguja wamesema kuwa ni vyema katiba mpya ya
Tanzania ikaainisha uwepo wa serikali tatu ili kuondokana na kero za Muungano
zilizopo hivi sasa.
Wananchi
hao walieleza hao jana huko Muyuni, wakati kamati ndogo ya Tume ya kukusanya
maoni ya katiba mpya ilipofika kijijini hapo.
Walisema
kuwa kumekuwepo na kero nyingi za Muungano ambazo zimekuwa kilalamikiwa na kila
upande, hivyo uwepo wa serikali tatu itazifanya kero hizo ziwe historia kwani
kila upande utashughulikia mambo yake na yale ya Muungano kushughulikiwa na
serikali hiyo.
Kwa
upande wake Pandu Issa Pandu alipendekeza uwepo wa serikali tatu ikiwemo kurudi
kwa serikali ya Tanganyika, Zanzibar
na serikali ya Muungano ambayo itakuwa ndio msimamizi mkubwa wa Serikali zote
mbili.
''Ninapendekeza
tuwe na serikali tatu yaani ya serikali ya Tanganyika,
Zanzibar na Serikali ya Muungano ambayo itakuwa
ndio msimamizi wa serikali zote mbili na hizo mbili ziwe huru na zijitegemee
kwenye mambo yake ya ndani'', alisema Pandu Issa Pandu (43).
Aidha
ambali ya kujitokeza maoni hayo pia wapo wananchi wa shehia hiyo waliopendekeza
Rais wa Zanzibar awe na madaraka kamili kuliko
ilivyo hivi sasa.
Walisema
mfumo uliopo hivi sasa unafanya kuonekana Tanzania
kuwe na rais mdogo na rais mkubwa, hivyo Rais wa Zanzibar
apewe mamlaka kamili.
Wananchi
hao pia walitaka mfumo wa mambo ya nje ubadilike utoe nafasi kwa Zanzibar nayo kutambulikana nje, hali inayoifanya kuweza
kunufaika zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.
Naye
Mwalimu Shukuru Ramadhani (28), akitoa maoni yake alisema suala la elimu ya juu
lifutwe kwenye mambo ya Muungano kwani Zanzibar
hainufaiki nalo.
''Tunataka
suali la elimu ya juu lisiwe la Muungano na wizara ya Elimu ya Zanzibar
iwe na Baraza lake la Mitihani, kwani tunahisi hatutendewi haki na Baraza la
Elimu juu liliopo hivi sasa la Muungano'', alisema Mwalimu Shukuru Ramadhan.
Suali
la elimu ya juu pia lilichangiwa na wanafunzi wa skuli ya Muyuni ambapo
walitaka suala la elimu lienguliwe kwenye mambo ya Muungano, huku wakieleza
kuwa NECTA inawadhulimu.
pongezi zenu wananchi wa Muyuni
ReplyDelete