Habari za Punde

Mazishi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu Mstaafu wa Hesabu za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Mohd Aboud Mohd { Mfaransa }

 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walipohudhuria mazishi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu mstaafu Mohammed Aboud Mohammed wengine kwenye picha na Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal na  Mwenyekiti wa mfuko wa Mwalimu Nyerere, Mhe Salim Ahmed Salim
 Waumini wakijumuika katika Sala ya Maiti iliyosaliwa katika msikiti wa ngazija
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib  Bilali, Makamu wa Pili wa Rais Wa Znzibar Balozi Seif Iddi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam  Desemba 29, 2012

Rais wa Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika mazishi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu mstaafu Mohammed Aboud Mohammed
 
Na Othman Khamis Ame
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Mstaafu wa Hesabu za Serikali wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa  Tanzania Bwana Mohd Aboud Mohd aliyefariki Dunia Nchini India  amezikwa katika makaburi ya Wangazija yaliyopo Kisutu Mjini Dar es salaam.
Mamia ya waislamu, familia, wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za  Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania walihudhuria mazishi hayo wakati wa jioni.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wake Dr. Mohd Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa SMT walikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi hayo.
Marehemu Mohd Aboud Mohd maarufu Mfaransa  alizaliwa Zanzibar Tarehe 25/1/1927 na kupata elimu zake za Dini na Dunia na alipomaliza masomo yake ya sekondari aliajiriwa serikalini mnamo tarehe 1/1/1944.
Marehemu Mohd Mfaransa kwa umahiri wake wa utumishi serikalini alipata fursa ya kupandishwa daraja hadi kufikia kuwa msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  hadi mwanzoni mwa mwaka 1967.
Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume alimpendekeza Mzee Mohd Mfaransa  kushika wadhifa wa Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 1/3/1967.
Tarehe 16/10/1967 Marehemu Mohd Mfaransa  aliteuliwa rasmi Mtanzania na Mwafika wa kwanza  baada ya Uhuru wa kuwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wadhifa aliokuwa nao hadi kustaafu kwake tarehe 25/12/1987.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Matehemu mzee Mohd Aoud Mohd    {Mfaransa }  mahala pema peponi amin.

2 comments:

  1. Mbona inashangaza kuona kiongozi wetu wa taifa anachekacheka msibani.kulikoni?

    ReplyDelete
  2. Ni moja ya tatizo ya viongozi bali jamii kwa jumla kushindwa kuelewa au kuelimishwa jinsi ya kuwa katika kila sehemu au kila tukio.

    Niliwahi kwenda mazikoni hapa UK ambapo kijana kutoka nyumbani alifariki na alikuwa na wenzake kutoka kazini na marafiki.

    Tulipofika makaburini tulikuta watu wengi sana si waislami ila wametulia kimya na hakuna anaezungumza.

    Tulipofika sisi shughuli ya mazungumzo ikaanza kwa upande wetu lakini wao wako vile vile kimya.

    Nikapata fundisho kubwa kwamba wenzetu wanaheshimu taratibu sisi hatuna utamaduni huo si kwamba hatunazo bali zipo ila kuziheshimu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.