Habari za Punde

Ujenzi wa Barabara Amani Mtoni Ukiendelea Utuaji wa Lami Awami ya Pili ya Mradi huo.

 Mafundi wa Idara ya Ujenzi wa Barabara wakiweka lami katika barabara ya Amani Mtoni ambayo ilikuwa ujenzi wake umesimama kwa muda mrefu, baada ya kujengwa awamu moja na kumaliziwa awamu ya pili ya mradi huo wa barabara inayojulikana kwa jina la Mkapa Road, ukiendelea na ujenzi wake wakiwa katika eneo la Redio One kuelekea Mtoni kuweka lami hiyo ili kuimarisha miundombinu ya barabara Zanzibar. 
 Hapa haiko sawa ngoja niweke sawa.

2 comments:

  1. Napinga upewaji wa majina yasio na tija kwa barabara zetu hapa Zanzibar.
    Barabara hii kuitwa jina la mkapa ni kosa.
    Ni vyema likaachwa jina lake la asili kuliko kupandikishwa jina la kiongozi ambaye ana damu ya wazanzibari mikononi mwake.
    Pia ni kiongozi anayetajwa sana katika watu waliojitajirisha kinyume cha sheria.
    Barabara hii iendelee kuitwa jina lake la asili.Please!

    ReplyDelete
  2. Jina la Mkapa limetolewa kwa sababu alipokuwa Rais alitoa fedha yeye au alitoa amri ya kutolewa fedha ya kujengwa barabara hii. Pesa za kujengwa barabara yote zilitolewa ila miaka yote ilipita na barabara haikumalizika mpaka kaingia Kikwete kawa Rais na bado barabara haijesha. Ile pesa ilikwenda wapi wakati ilikwishatolewa??? Pesa inayojenga barabara hii leo si ile iliyotolewa na Mkapa. Na hakuna aliyechukuliwa hatua kwa hili kwa barabara ile kubakia katika hali ile zaidi ya miaka kumi!!! Hii ndiyo Zanzibar njema

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.