Kikosi cha Miembeni |
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imetolewa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya sare ya bila kufungana na Miembani FC jioni hii kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung, Zanzibar.
Matokeo hayo yanaifanya Miembeni isubiri hatima yake ya kuingia Nusu Fainali katika mchezo wa usiku wa leo kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Miembeni sasa ina pointi nne, baada ya kumaliza mechi zake tatu ikiwa katika nafasi ya pili, nyuma ya Azam inayoongoza Kundi A kwa pointi nne pia na wastani mzuri wa mabao.
Timu tatu sasa zina nafasi ya kuingia Nusu Fainali, Miembeni yenye pointi nne sawa na Azam na Mtibwa Sugar ambayo ikiwa na pointi moja hivi sasa, ikishinda usiku itatimiza pointi nne na mustakabali wake wa kusonga mbele utatazamwa kutokana na wastani wake wa mabao.
Tayari kutoka Kundi A, mabingwa wa Kenya, Tusker FC wamefuzu kama vinara wa kundi hilo, wakati Simba SC, mabingwa wa Bara wamefuzu kama washindi wa pili.
Mshindi wa kwanza wa Kundi A atamenyana na mshindi wa pili wa Kundi B katika Nusu Fainali, wakati mshindi wa kwanza wa Kundi B atamenyana na mshindi wa pili wa Kundi A.
No comments:
Post a Comment