Habari za Punde

Mapinduzi Cup Coastal Union na Miembeni

Mchezaji wa timu ya Coastal akimpita beki wa timu ya miembeni wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi, timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana,


Kizaaza katika goli la timu ya Miembeni katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi.

Muamuzi wa mchezo kati ya Miembeni na Coastal Mpoma akimshindikiza mchezaji wa timu ya miembeni kuokoa muda ili kuendelea na mchezo huo uliofanyika uwanja wa Mao.


Beki wa timu ya Coastal Khamis Shengo kushoto na mshambuliaji wa timu ya Miembeni Peter Ilunda wakiwania mpira katika mchezo Kombe la Mapinduzi, timu hizo zimetoka sare.
Mshambuliaji wa timu ya Miembeni Peter Ilunda akimpita beki wa timu ya Coastal Ismail Suma.
Mshambuliaji wa timu ya Coastal Suleiman Kassim, akipiga mpira golini kwa timu ya miembeni huku kipa wa timu ya miembeni akiokoa mpira huo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.