Na Andrew Chale
MWAKILISHI wa Jimbo la Bububu, Hussein Ibrahim Makungu, anatarajia kutimiza
ahadi zake kwa kutoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 248 pamoja na
fedha taslimu sh milioni 50 kwa ajili ya maendeleo jimboni humo.
Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza Mwakilishi huyo atatoa vifaa
hivyo Jumapili ijayo katika hafla ambayo pia itahudhuriwa na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd.
Taarifa hiyo ilieleza baadhi ya vifaa atakavyokabidhiwa ni gari moja la
wagonjwa, gari kubwa aina ya Fuso, basi moja aina ya Coaster, magari mawili aina
ya Carry maalumu kwa ajili ya kuzolea takataka na matanki makubwa 20 ya lita
5,000.
Vitu vingine atavyofanya mwakilishi huyo ni kujenga minara 20 kwa ajili ya
kuwekea matanki ya maji, mipira tisa kwa ajili ya kupitisha maji, vigari vya
walemavu 10, pikipiki aina ya Vespa tano ambazo zimeshalipiwa bima, televisheni
tano, ving’amuzi vitano na makochi jozi tano.
Makungu alisema vifaa hivyo anavitoa ikiwa ni kutimiza ahadi alizotoa wakati
wa kampeni za uchuguzi mwaka jana.
“Mara nyingi wengi wanaahidi vitu vingi na baadaye kushindwa kutekeleza au
kusubiri wakati wa kampeni za uchaguzi ndio watekeleze ahadi zao, mimi nataka
kuwaambia wakazi wa jimbo langu kuwa nawajali sana na ahadi zangu zote
nitazitekeleza mapema…ni miezi michache toka waliponichagua kuwa mwakilishi wao
na tayari nimetimiza karibu robo tatu ya ahadi zangu kwao,” alisema Makungu.
Cahnzo - Tanzania Daima
Lazima tuwe makini na hii misaada.Ni lazima kutaka kujuwa wapi mapesa haya yanapotoka,tunalishwa haramu na tunakubali waislamu na ni njia moja ya kuwarubuni wenye njaa na wasokuwa na elimu ya dini.
ReplyDeleteJeee Mtoto wa miaka 14 aliopigwa risasi ya moto katika kuwania jimbo la Bububu Mh Muwakilishi wakuteulia samani ya Roho yake ni kiasi gani?
ReplyDeleteFanya kwanza umridhishe Allah sio kutowa na ukajisifu.
labda tuulize mshahara wa Mwakilish iwa ZNZ ni bei gani na hii kama si pesa ya Hazina inayochotwa kwa mlango wa Nyuma wa CCM
ReplyDelete