Habari za Punde

Mwakilishi wa bububu kutimiza ahadi Jumapili

Na Andrew Chale
 
MWAKILISHI wa Jimbo la Bububu, Hussein Ibrahim Makungu, anatarajia kutimiza ahadi zake kwa kutoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 248 pamoja na fedha taslimu sh milioni 50 kwa ajili ya maendeleo jimboni humo.
Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza Mwakilishi huyo atatoa vifaa hivyo Jumapili ijayo katika hafla ambayo pia itahudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd.
Taarifa hiyo ilieleza baadhi ya vifaa atakavyokabidhiwa ni gari moja la wagonjwa, gari kubwa aina ya Fuso, basi moja aina ya Coaster, magari mawili aina ya Carry maalumu kwa ajili ya kuzolea takataka na matanki makubwa 20 ya lita 5,000.

Vitu vingine atavyofanya mwakilishi huyo ni kujenga minara 20 kwa ajili ya kuwekea matanki ya maji, mipira tisa kwa ajili ya kupitisha maji, vigari vya walemavu 10, pikipiki aina ya Vespa tano ambazo zimeshalipiwa bima, televisheni tano, ving’amuzi vitano na makochi jozi tano.
Makungu alisema vifaa hivyo anavitoa ikiwa ni kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchuguzi mwaka jana.
“Mara nyingi wengi wanaahidi vitu vingi na baadaye kushindwa kutekeleza au kusubiri wakati wa kampeni za uchaguzi ndio watekeleze ahadi zao, mimi nataka kuwaambia wakazi wa jimbo langu kuwa nawajali sana na ahadi zangu zote nitazitekeleza mapema…ni miezi michache toka waliponichagua kuwa mwakilishi wao na tayari nimetimiza karibu robo tatu ya ahadi zangu kwao,” alisema Makungu.
 
Cahnzo - Tanzania Daima

3 comments:

  1. Lazima tuwe makini na hii misaada.Ni lazima kutaka kujuwa wapi mapesa haya yanapotoka,tunalishwa haramu na tunakubali waislamu na ni njia moja ya kuwarubuni wenye njaa na wasokuwa na elimu ya dini.

    ReplyDelete
  2. Jeee Mtoto wa miaka 14 aliopigwa risasi ya moto katika kuwania jimbo la Bububu Mh Muwakilishi wakuteulia samani ya Roho yake ni kiasi gani?

    Fanya kwanza umridhishe Allah sio kutowa na ukajisifu.

    ReplyDelete
  3. labda tuulize mshahara wa Mwakilish iwa ZNZ ni bei gani na hii kama si pesa ya Hazina inayochotwa kwa mlango wa Nyuma wa CCM

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.