Na Mwandishi wetu
WAZEE
wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar wamempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, kwa kuadhimisha kwa miaka 49 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Wazee
hao walisema maadhimisho hayo yalikuwa na mafanikio sambamba na kushuhudiwa
hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Wazee
hao walisema utekelezaji wa kauli ya CCM ya Mapinduzi Daima ilitafsiriwa kwa
vitendo kuboresha maendeleo ya nchi na wananchi.
Walisema
uzinduzi wa miradi ya skuli za kisasa,
vituo vya afya, uboreshaji wa nyumba za wazee, barabara za kisasa, madaraja,
upanuzi wa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji maji, majengo ya afisi za serikali
ni hatua moja ya kufikiwa maendeleo hayo.
Aidha
walimsifu Dk. Shein kwa kuendelea kusimamia vyema serikali yake yenye mfumo wa
umoja wa kitaifa.
No comments:
Post a Comment