Habari za Punde

Kashfa matokeo ya kidato cha nne: Watahiniwa wamchora Messi wawapiga vijembe wabunge

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
 
Fredy  Azzah, Joyce Mmasi

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.

Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo fleva).

“Mwaka jana tulikutana na ‘single’ yaani waliandika mashairi kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu, wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima kumlalamikia mpenzi wake. Miongoni mwa yaliyoandikwa ni mpenzi, umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…” alisema Dk Ndalichako.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine waliandika malalamiko  dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge.

“Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…” alisema.

Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya.

Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao waliviita Messi (Lionel, mchezaji wa Barcelona) na zombi (ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa kwenye televisheni.

Sababu za kufeli
Dk Ndalichako alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya kwa nini matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya, lakini akadokeza kuwa huenda yametokana na wanafunzi wengi kukosa maarifa.

Anasema mbali na waliojaza matusi na michoro, wanafunzi wengine waliofanya vibaya ni wale ambao hawakujaza chochote kwenye karatasi zao za majibu.

“Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza.”

Dk Ndalichako alisema kwa ku mbukumbu zake, hakuna matokeo mabaya kama ilivyo kwa mwaka huu yaliyowahi kutokea.

“Tukiangalia tu kuanzia 2000, hakujawahi kutokea matokeo mabaya kama haya, kwa kweli hali haipendezi. Hata kabla ya kuyatangaza nilikuwa nayaangalia mara tatu tatu, sikuyapenda na inasikitisha kwa kweli,” alisema Dk Ndalichako.
 
Chanzo: Mwananchi

6 comments:

  1. HIVI HAWA WANAFUNZI WA TANZANIA AU WALOWEAJI?HIVI KWELI UNALIPA PESA MIAKA MINNE HALAFU MTOTO ANAFELI KUPITA KIASI KISA KASOMA SHULE ZA KATA.WATOTO WALIOTOKA MEDIUM SCHOOL WENGI WALIPANGIWA HIZO ILIWAFELI TU!IWEJE SHULE BINAFSI ZINA MATOKEO MAZURI?NANYIE MLIOSAHIHISHA MTIHANI MLIKUWA NA MPANGO GANI?MHESHIMIWA RAISI J K MBONA UKO KIMYA KAKA YANGU HIVI WATOTO TUWAPELEKE WAPI?TUSAIDIE BABA HATA IKIBIDI MITIHANI ISAHIHISHWE TENA HATA WENYE AKILI WAMETOKA OLA!UUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUiiiiiiiiiiiiiiii NDUGU YANGU KIKWETE NACHANGANYIKIWA JAMANI TUSAIDIEEEEE

    ReplyDelete
  2. ENYI WAALIMU MNAODAI HAKI ZENU BILA KUKUMBUKA WANAFUNZI ILA KUAGIZA VIFAA KIBAO NA HELA ZA MIKAKATI LUKUKI HALAFU WATOTO WANARUDI PATUPU KWELI HAMNA HURUMA HATA CHEMBEE.ZAIDI HAYO MAJEMBE CHELEWA NDOO MAFYAGIO NI MALI YA KUTOSHA KUJAZA HARDWARE NA MNAGAWANA KILA MWAKA HUKU SIFURI ZIKIONGOZA MASHULENI JAMANI HAMJISIKII VIBAYA NA WATOTO MNAWATUMIKISHA VYA KUTOSHA BILA KUJALI MAADILI YAO WE MWALIMU UJUE MUNGU YUKO NA KWAKE KUNA MAISHA TENA SASA WEWE ITAKUWAJE?TUNATOA SHUKURANI NYINGI KWA WAALIMU WOTE WA SEREKALINI KWA KAZI NZURI MLIOFANYIA YA KUSABABISHA WANAFUNZI WAJIU NA KUTOROKA MAJUMBA KISA MATOKEO MABAYA.DAMU ZA WALIOJIUWA NA ZIWE JUU YENU.

    ReplyDelete
  3. MHESHIMIWA WAZIRI WA ELIMU USIEENDELEE KUREMBA HUO MZOGA WA ELIMU TOA UFUMBUZI WA HAWA WATOTO WANAOZAGAA MTAANI BAADA YA KUFELI IWEJE? SIJUI UNASUBIRI NINI AU WA KWAKO WANASOMA SHULE BINAFSI HIVYO HUNA SHIDA NA UNAJIWEZA KWA MSHAHARA MKUBWA TUNAOKULIPA SISI AMBAO WATOTO WETU HAWANA PAKWENDA UKWELI JITAHIDI MITIHANI ISAHIHISHWE TENA NA SWALA LA KUKATA RUFAA NA KULIPIA 20000 KWA KILA SOMO LITAKALO RUDIWA KUSAHIHISHWA LISAHULIKE HUO NDIYO UFISADI TUSIOTAKA HAKI ITENDEKE ILIASIEKUWA NA UWEZO NAE APATE HUDUMAAAA.FOMU ZA RUFAA MWIKO!TUNAMLILIA MUNGU MPAKA HAKI ZETU TUPEWE HAKUNA ANAEMSHINDA MUNGU IKO SIKU ATAWEKA MAMBO HADHARANI NDIPO KILIO KIKUU KITASIKA KUTOKA KWA WANAOTUNYANYASA WALALAHOI MAANA NI MUNGU ALITUUMBA WALA SIO HAO WALAKU WA MAISHA NA DUNIA!

    ReplyDelete
  4. NA NYIE WABUNGE MSITULETEE ZA KULETA MNAFANYA NINI HAPO DODOMAA? HAKIKISHENI MITIHANI INARUDIWA KUSAHIHISHWA BILA GHARAMA YOYOTE ILI SISI TULIOWACHAGUA TUONE UMUHIMU WENU.AMKENI WOTE NENDENI WIZARA YA ELIMU MKASIMAMIE USAHIHIJASHI WAHESHIWA MNAJISAHAU HAMJUI BILA SISI HAPO BUNGENI HAMKANYAGI?AU NANYIE MNASHIRIKI UHARIBIFU WA KUIUWA TANZANIA?ACHENI MASIHARA WENGINE HUKU MAMBO NI MABAYA SANA KAMA HIVI TUNAZIKA WATOTO WETU WALIOKUWA NA BIDII WAKIWA NA MATARAJIO YA KUSOMA ZAIDI HATA WAWE VIONGOZI KAMA NINYI LAKINI LEO ARIDHI IMEWAMEZA JAMANI!OK YAWEKANA MPANGO NI WATOTO WA VIONGOZI WAJE KUSHIKA MADARAKA KWA KUWA WAO HAWASOMI HUKO KATA TENA WAKO NJE YA TANZANIA ILA PATA CHIMBIKA HILO MLIELEWE KABISAAAAAAAAA!

    ReplyDelete
  5. HALAFU WEWE ULIETOA UTARATIBU WA KUSAHIHISHA TENA MITIHANI KWA KUKATA RUFAA NA KULIPIA ELFU ISHIRINI KILA SOMO FUTA HARAKA HILO TANGAZO SISI SIO WALOWEZI ELEWA TUNALIPA KODI SANA KWA KUKATWA MISHAHARA JAPO NA KIMA KIDOGO KISICHOONGEZWA KWA MUDA MREFU.HUO NI UNYANYASAJI WA HALI YA JUU SANA NA MRADI WA ULAKU WA MAISHA.TUACHE BWANA SISI NI WAZALENDO WA TANZANIA.JAMANI RAISI TUSAIDIE TUNAULIWA MBALI HUKU UNATUANGALIA KABISAA BABA NASI NDIYO TULIOKUCHAGUA JAMANI JK!

    ReplyDelete
  6. HIVI HATA UONGOZI WA CHAMA TAWALA MNALIFUNGIA MACHO NDUGU ZANGUNI HEBU KOHOENI TU HUU MTIHANI USAHIHISHWE TENA JAMANI!NYIE NDIYO MHIMILI WETU SASA MKO WAPI?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.