Habari za Punde

Kibaka wa Viatu Msikitini Apata Kibano

 Kijana akiwa hui baada ya kupata kipigo kutoka kwa Wananchi wenye ahasira baada ya kumkamata akiiba viatu katika msikiti wa Rahaleo wakati wa sala ya Alasiri leo, alijifanya na yeye ni mmoja wa muumini akisali baada ya kutowa salamu akafanya kazi yake hiyo ya kukomba viatu vya wananchi waliohudhuria sala katika msikiti huo.

 Wananchi wakimsachi kijana huyo baada ya kutembeza kipigo na kumkuta na nyongo za bangi karibu 15 akiwa nazo mfukoni mwa suruali yake, la kushangaa hajuwi nini anafanya akisali na nyongo za bangi, hii si lana  na kufika arubaini yake na kupata kipigo hicho.

Kijana aliyekamatwa akiwa na rasketi iliyojaa viatu alivyoviiba katika msikiti wa rahaleo ikiwa ya mmoja ya mwananci aliyekuwa akisali katika msikiti huo. Ilibidi wasamaria wema kumuombea baada ya kmupata kipigo na wengine kulalamika kuwa hakutoka damu kwa nini aachiwe mpaka tumpasuwe huu aache kuiba katika misikiti 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.