Na
Maryam Salim, Pemba.
MSHITAKIWA,
Khamis Said Ramadhan ( 28) mkaazi wa Vikutani- Vitongoji Wilaya ya Chake Chake
Mkoa wa Kusini Pemba ,amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Chake Chake
kujibu shitaka lake la kuvunja na kuiba magodoro 4 katika Chuo cha Mafunzo ya
Amali Vitongoji .
Kwa upande wa hati ya Mashtaka
iliyowasilishwa Mahkamani hapo , ulidai mbele ya Hakimu, Omar Mcha Hamza, kuwa siku ya Jumamosi
muda usiojulikana ya Agosti 25 mwaka huu,
alitenda kosa hilo huko katika chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji ikiwa ni Mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Mshitakiwa huyo ilidaiwa kuwa aliiba
magodoro 4 ya futi sita kwa sita yenye thamani ya T.sh,360,000/=kwa makisio mali
ya kituo cha mafunzo ya Amali kilichipo Vitongoji .
Muendesha mashtaka kutoka Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka, Seif Mohammed Khamis, alidai Mahakamani hapo kuwa Mshitakiwa
huyo alitenda kosa hilo ikiwa ni kosa K/F cha sheria NO.6/2004 sheria ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa upande wa mashahidi 6 ambao ni, Ayoub
Magawe Habira ,Juma Mussa Ame,Juma Suleiman Saleh ,Salim Ali Mbarouk ,Fatma Ali
Khamis na D3399 D/C sajent Juma ,tayari walishapandishwa na kutoa ushahidi juu
ya tuhuma hizo.
Mashahidi hao walidai kuwa, mshitakiwa huyo
hawakumuona kuvunja wala kuiba bali walipata taarifa kutoka kwa mnunuzi, ambaye
ni Salim Ali Mbarouk alidai kuwa aliuziwa Godoro moja kutoka kwa kijana huyo
kwa bei ya Tsh,5000/= bila ya ushahidi bila risiti kutoka kwa muuzaji, kwa
sababu alimueleza kuwa anashida.
Khamis
Said Ramadhan, alipotakiwa kujibu shitaka lake, mahakamani hapo alikana ushahidi uliotolewa na Askari Upelelezi, kwani
siku hiyo alidai hakuwepo katika eneo la tukio ,na kuiambia Mahakama kwamba Magodoro
yaliyoibiwa ilidaiwa ni 4, lakini lilikamatwa ni moja, aliiuliza mahakama hiyo
na kuiomba mahakama iyangalie kwa vyema ushahidi ambao umetolewa.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Omar Mcha
Hamza aliihairisha kesi hiyo hadi Septemba 11mwaka huu.
No comments:
Post a Comment