Na Laifat Kassim, Pemba.
MAHAKAMA ya mkoa wa Chake Chake,
imempandisha katika Kizimba cha Mahakama , Abubakar Mkulu Bakar [28] mkaazi wa
Wambaa, Mkoa wa Kusini Pemba, kujibu tuhuma ya kuwabaka watoto wawili wa kike
[13] kila mmoja ( Mapacha) wakaazi wa Msuka
Mtoni Wilaya ya Micheweni.
Kitendo hicho kilichofanywa na mtuhumiwa
huyo ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha
125 [1] [2] [e] na K/F cha 126 [1] cha sheria namba 6 ya mwaka 2004 sheria ya
Zanzibar.
Kwa mujibu wa hati za mashtaka
iliyowasilishwa Mahakamani hapo na Muendesha mashtaka kutoka Ofisi ya
mkurugenzi wa Mashtaka, Ali Bilali Hassan, mbele ya Hakimu, Khamis Ramadhani Abdalla, mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo,
baina ya mwaka 2011 na mwaka 2013 huko Wambaa Mkoani Pemba, Tanga na Mwanza -Tanzania
Bara kwa makusudi ambapo aliwabaka
watoto hao na kuwasababishia maumivu sehemu ya siri, jambo ambalo ni kosa kisheria.
Baada ya kusomewa waraka huo, Mshtakiwa
alikataa kuwafanyia kitendo hicho isipokuwa alikiri kuwa Watoto hao alikuwa nao.
“Mimi toka niwachukue watoto hao sijawahi
kuwafanyia hata siku moja kitu hicho na nilikuwa ninawalea kama watoto wangu
niliwowazaa”alisema .
Kwa upande wa Shahidi namba moja ambae ndie
baba wa mapacha hao mkaazi wa Msuka, alidai kuwa aliwachukuwa kwani alimpa watoto wake wakati
yeye akiwa ni Mgonjwa.
“Kwa kweli kijana huyu aliizoea kwangu
nakuniambia ni Mganga wa kutengeneza dawa, kwa vile nilikuwa ni mgonjwa wa
vidonda vya tumbo alinitengenezea Dawa nikanywa, baada ya kunywa maradhi
yalizidi na kuondoka na watoto wangu” alidai.
Alidai baada ya kuondoka na watoto hao
alikuwa anawasiliana naye na baadae
mawasiliano yakakatika kwa muda wa miezi sita[6] na baadae aliamua kumfuatilia
mshtakiwa huyo kwenda Tanga kuwaona watoto wake ingawa hakufanikiwa.
“Baada ya kushauriana na mke wangu
na kujenga wasiwasi mkubwa kwa watoto wangu niliuza ng’ombe na kwenda Tanga
kuwachukuwa watoto wangu nilipofika simu ikazimwa na sikuipata tena,
niliwatafuta lakini sikuwaona nikarudi” alidai.
Kwa upande wa shahidi namba mbili ambae ni
baba mdogo wa mapacha hao aliiambia mahakama kuwa, mtuhumiwa huyo baada
ya kukamatwa na kupelekwa Polisi na baadae kwenda Hospitali kwa ajili ya vipimo
vya watoto hao na kuonekana wameharibiwa alimwambia kuwa, yalopita yamepita,
hivyo nakuomba unisamehe.
“Baada ya kipimo kuonesha watoto wameharibiwa, aliniambia nimsamehe na ataniandikia kipande cha shamba au atanipa
pesa ninazotaka”Alieleza.
Baada ya ushahidi huo nao kati wa mapacha
hao ambae ni shahidi namba tatu alidai
kuwa, nikweli alikuwa anawafanyia uovu huo, na kabla ya kuwafanyia alikuwa
anajipaka mafuta au mate katika sehemu zake za siri na baadae kuwaingiliza
sehemu za siri za mbele kwa zamu.
“Sisi alikuwa anatuambia tuende Kisimani na
mmoja abakie na nikibakia ananivua nguo na kunifanyia udhalilishaji huo na
alikuwa anatufanya kwa zamu na akimaliza alituambia tusiseme” Alieleza Shahidi
huyo.
Nae shahidi namba nne ambae ni mmoja kati
ya mapacha hao, aliiambia mahakama kuwa, alikuwa anawambia yeyote ambae
atawauliza waseme kuwa ni baba yao wa kuwazaa na kama hawakusema alikuwa
anawapiga.
“Kila ambae anatuuliza tulikuwa tunasema ni
baba yetu alotuzaa na siku ambayo tumekosea hatukusema hivyo akisikia alikuwa
anatupiga bakora” alisema Shahidi huyo.
Baada ya ushahidi huo, mshtakiwa alijitetea
na kuiambia Mahakama anaomba dhamana, lakini Hakimu wa Mahakama hiyo, alimuambia
kama atapata wadhamini madhubuti ataweza kupata dhamana na kabla ya dhamana awe
na Shilingi milioni moja [1000,000/=] taslimu na wadhamini wawili.
Kesi hiyo imehairishwa hadi Juni 5 mwaka
huu kwa kuwasikiliza mashahidi wengine, ambapo Mtuhumiwa huyo alirudishwa Rumande.
asipewe dhamana wala waraka huyo anastahili afungwe tena kifungo cha miaka isiopungua 40 ili akitoka asiwe na nguvu ya kudhalilisha watoto wetu wengine.. mtovu wa adabu asokua na adabu... mjaalana mkubwa....
ReplyDeleteSubhanallah lakini watu wataacha lini mambo haya ya kuaminiana mpaka kumpa mtu watoto wako .
ReplyDelete' No country for oldmen '