Habari za Punde

Dk Afanya uteuzi wa Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa usajili biashara na mali

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI    17/06/2013
 
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. ALI MOHAMED SHEIN AMEMTEUA BWANA ABDULLA WAZIRI RAMADHAN KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA WAKALA WA USAJILI BIASHARA NA MALI, ZANZIBAR.
 
UTEUZI HUO AMEUFANYA KWA MUJIBU WA UWEZO ALIOPEWA CHINI YA KIFUNGU NAMBA 6(1) CHA SHERIA YA WAKALA YA USAJILI WA MALI NAMBA 13 YA MWAKA 2012.
 
KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI AMBAYE PIA NI KATIBU MKUU KIONGOZI DKT. ABDULHAMID YAHYA MZEE,UTEUZI HUO UNAANZA JUNE 15 MWAKA 2013.
 
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

1 comment:

  1. Jamani hapa zbar hakuna vijana walosoma? niwale wale hawastafu, au ndio usultani, wa, kihadim, na hawa Cuf muamsho,ha wasemi wala hawahoji au kwa kuwa nawawo n ijamii hii ya kula kwenda mbele, jitu lina miaka 65 bado ndio kwanza ana teuliwa kupewa kula,nchi yenye watu milion moja na laki tano wakurugenzi bakati manaibu, mnatupeleka wapi?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.