Habari za Punde

Uchaguzi wa Udiwani Ng’ombeni Juni 23


Na Bakar Mussa, Pemba
TUME ya Uchaguzi Wilaya ya Mkoani Pemba, inatarajia kufanya uchaguzi mdogo wa kumchaguwa Diwani wa Wadi ya Ng’ombeni, kufuatia kifo cha aliekuwa Diwani wa Wadi hiyo, Massoud Khamis Omar.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Msimamizi wa uchaguzi wilaya hiyo,Seif Salim Juma, alisema uchaguzi huo unatarajiwa kufanywa Juni 23 mwaka huu na vyama vitatu vitashiriki.

Aliwataja wagombea hao kuwa ni Siwajibu Ali Khamis (CCM), Salum Abdalla Juma (CUF) na Hassan Matora Hussein (UDP).

Msimamizi huyo aliwataka wananchi wa wadi hiyo, kushiriki katika mikutano kampeni na kusikiliza sera za vyama vyote na baadae kuchagua mgombea wamtakae.

Alisema vituo vitakavyotumika ni vile vilivyotumika katika uchaguzi mkuu uliopita na sio vyenginevyo, na pale itakapotokea taarifa nyengine wananchi wataelezwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.