Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar na kuhudhuriwa na Wanachama wa CCM wa Mikoa minne ya CCM Unguja.
Kombando Dkt. Salmin Amour Juma, akiwasalimia wanachama wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti Zanzibar. hii ni mara ya kwanza kwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar kuhutubia katika hadhara kama hii na kushangiliwa na Wananchi na Wanachama wa CCM waliokuwa katika viwanja hivyo.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia Mkutano wa hadhara wa CCM katika viwanja vya Kibanda maiti.
Komandoo Dkt. Salmin Amour Juma akiwasilimia Wanachama wa CCM katika viwanja vya Kibanda maiti.
Mwananchi akichukua picha kupitia simu yake wakati wa mkutano wa hadjara wa CCM.
Mzee Ali Ameir akisalimia na kutowa Salamu za Wananchi katika mkutano huo
Naibu Katibu Mkuu wa ccm Zanzibar Vuai Ali Vuai, akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya kibanda maiti Unguja na kuhudhuriwa na Wanachama wacCCM wa Mkoa Minne ya CCM Unguja.
Mwenyekiti wacCCM Mkoa wa Mjini Silima Borafya akizungumza katika mkutano huo.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti Unguja.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Alhaj Mwangi Ramadhani Kundiya, akisoma risala ya WanaCCM wa Mkoa Minne ya Unguja katika mkutano huo uliohutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika viwanja vya Kibanda Maiti.
ndugu yangu salimini bado unakumbatia dunia? hayo yaliyokufika bado tu hayajatosha?
ReplyDeleteNeno "harama" linatumika katika kiswahili cha Tanganyika/Bara na neno "Nkataba" likitilia mkazo au kuanisha kiswahili cha kisiwani Pemba......Naishia hapa na uchambuzi huu.
ReplyDeleteKama haikuwa shina itakuwaje mizizi hawa viongozi walopanda jukwaani jana wamepitwa na wakati, au ndio ccm, inaonesha wazi kuwa imeishiwa na watendaji imara wenziwao ,Cuf uamsho wana wabomowa kwa nguvu ya hoja wao wana tapatapa, mbona karume mdogo hawaku mualika yeyendie mwenye mvuto kwa kizazi kipya;wana mkumbuka leo kamando maji yashazidiunga
ReplyDeleteMaskini chama langu!
ReplyDeleteUongozi mbovu wa chama Z'bar, na kukifanya chama kuwa mradi wa watu kutafutia kazo watoto wao imetugharimu!
Na kama viongozi hawatobadilika, huenda Vuai chama kikamfia mikononi!
CCM itakufa kifo cha mende kwani kinamalizia waladhwaliina Wazanzibari wameikataa CCM since uchaguzi wa Abdul Wakil Nombe kabla ya vyama vingi.
Delete