Spika waBaraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Pandu Ameir Kificho akifungua semine ya siku moja juu ya Ugunduzi wa Mafuta na Gesi wa Haidrokaboni katika bahari ya kina kirefu, semina hiyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa baraza chukwani.kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kulia Makamo wa Rais wa kampuni ya Shell Sub Sahara Afrika Dr.Alastair Milne.
Mtoa mada ya uchimbaji wa Mafuta na Gesi Menno de Ruig PhD.akitowa maelezo ya uchimbaji wa mafuta na gesi kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati wasemina ilioandaliwa naKampuni hiyo kutowa uelewa na shughuli za uchimbaji.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika semina ya ugunduzi wa mafuta Zanzibar iliokuwa ikitolewa na Kampuni ya Shell kwa wajumbe hao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza muwezeshaji katika semina ya ugunduzi wa mafuta na gesi iliotolewa na kampuni ya Shell.
Wajumbe wakifuatilia mada zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Shell Sub Sahara Afrika Dr.AlastairMilne.akionesha michoro katika semina hiyo kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi chukwani.
Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa. akifuatilia mijadala katika semina ya Ugunduzi wa mafuta na gesi katikabahari kuu.
Mwakilishi wa Kwamtipura Hamza Hassan, akichangia katika semina hiyo baada ya kuwasilishwa mada na wataalam kampuni ya Shell.
Mtaalam wa Uchimbaji wa Mafuta Eng. Ali Bakari, akichangia katika semina hiyo, iliowashirikishwa Wajumbe waBaraza la Wawakilishi wa Maofisa wa Nishati Zanzibar.
Mwakilishi waa Kuteuliwa na Rais Juma Duni , akichangia mada katika semina hiyo juu ya Ugunduzi wa Mafuta na Gesi katika bahari ya kina kirefu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Fatma Ferej akichangia katika semina hiyo.
Dkt. Alastair Milne akifafanua na kujibu michango iliowashilishwa katika semina hiyo na wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya ugunduzi huo.
Makamuo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi , akifunga semina ya siku moja iliohusu Mafuta na Gesi Zanzibar. ilioandaliwa na Kampuni ya Kimataifa ya Shell, semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa baraza la wawakilishi Chukwani.
No comments:
Post a Comment