Mkurugenzi wa Zantel, Pratpa Ghose akiongozana na Afsa Rasrimali watu, Francis Kiaga
Wafanyakazi wa Zantel wakichukua chakula
Wafanyakazi wa Zantel wakijumuika kupata futari
Zantel yawafuturisha wafanyakazi wake
Akizungumza na wafanyakazi hao wakati wa hafla hiyo Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Zantel, Bwana Pratap Ghose aliwataka wafanyakazi hao
kuimarisha urafiki na upendo kati yao.
Alisema kuwa katika kipindi hiki cha mfungo wafanyakazi wakiwa
kama waumini wengine wa dini ni vema wakatambua kuwa kipindi hiki cha mfungo ni
kipindi cha kukaa pamoja na kutafakari mazuri ambayo wanatakiwa kuyafanya kati
yao pamoja na jamii nzima inayowazunguka.
“Hiki ni kipindi muhimu sana kwetu wafanyakazi wote kwa
ujumla katika kujitafakari kwa kiasi gani tumeishi katika jamii zetu na wenyewe
kwa ujumla huku tukijiimarisha zaidi katika imani zetu za kidini” alisema
Pratap.
Katika hafla hiyo wafanyakazi hao walipata wasaha wa
kuulizana maswali yahusuyo utendaji wa kazi zao pamoja na maswali mengine ya
chemsha bongo.
No comments:
Post a Comment