Watoto wengi hupenda kusheherekea sikukuu kwa kutumia michezo mbali mbali, ambayo huwavutia na kuwafurahisha, kama wanavyoonekana katika picha, watoto wakiwa katika pembea, kwenye kiwanja cha Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
Watoto wengi hupenda kusheherekea skukuu kwa kutumia michezo mbali mbali, ambayo huwavutia na kuwafurahisha, kama wanavyoonekana katika picha, watoto wakiwa katika pembea, kwenye kiwanja cha Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
Ipo haja kwa serikali kuviimarisha viwanja vya kufurahishia watoto, hususana katika maeneo ya mbali mbali kisiwani Pemba, kama wanavyoonekana katika picha, watoto wakiwa katika kiwanja cha Mchanga Mdogo wakisheherekea skukuu ya Idd ell Fitri jana jioni. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba)
Pemba imetupwa sana, jamani not fair, inakuwaje viwanja vya watoto Unguja kama Jamuhuri na Kariakoo vinatengezwa na kuwa bora na kileo, pemba wamekutupa kabisa, inapofika wakati wa skukuu watoto na familia wanaenda Unguja kusherekea skukuu kwa vile pemba kumeboreteka kutokana na sherehe za eid.
ReplyDeleteTunaiyomba serikali iyangalie hilo, kutengeza viwanja wa sherehe kama skukuu hata pia viwanja vya kupumzika siku za kuwaida kama vile forodhani.
Yapo maendeo pemba tunaweza kutengeza kama vile forodhani , itasaidia kuinua uchumi wa nchi na utalii, pia itawafanya wananchi wa pemba nao kujisikia raha katika maisha yao pale wanapokwenda sehemu za mapumziko kujipatia vyakula pia kama vile forodhani.
MV SPICE ilio zama wakati ule ilibeba wananchi ambao karibia 3000 ambao wakitoka unguja kwenda pemba kwa kumaliza sherehe za eid, tunataka wananchio wa Pemba nao wanafurahia eid kama wananchi wa Unguja.