Habari za Punde

Trein Yagongwa

Na Mwandishi wetu DSM
KAMPUNI ya reli Tanzania (TRL) umesitisha huduma za usafiri katika jijini la Dar es Salaam baada ya kichwa cha treni kupata ajali.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa TRL, kichwa hicho kiligongwa na lori juzi saa 12:30 jioni katika makutano ya reli Buguruni.

Ajali hiyo imesababisha kuharibika kichwa cha treni na kuhitaji matengenezo kabla ya kuendelea na huduma.
Huduma za usafiri zilitarajiwa kurejea tena leo.
Hata hivyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.