Wafuasi wa CUF wakiwa wakibeba ujumbe mzito katika eneo la Donge.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muwanda Jimbo la Donge.
Vijana wa CUF Donge, wakighani utenzi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Muwanda Donge.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akipandisha bendera katika moja ya matawi mapya ya chama hicho katika eneo la Donge.Wafuasi wa CUF wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi kadi kwa mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho katika Jimbo la Donge.
Wafuasi wa CUF wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Picha na Salmin Said, OMKR
Na Hassan Hamad, OMKR
Hatimaye Chama Cha Wananchi (CUF) kimeingia katika kijiji cha Donge kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muwanda na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Maelfu ya wafuasi wa Chama hicho kutoka maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini walijitokeza katika mkutano huo ili kushuhudia kile kilichokosekana kwa muda mrefu kuingia katika eneo hilo la Donge kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.
Akizungumza katika mkutano huo, Maalim Seif amesema anajisikia fahari kuzungumza na wananchi wa Donge katika eneo la ndani la jimbo hilo.
Amesema Donge ni kijiji chenye historia ndefu na ambacho kimejipatia umaarufu mkubwa Zanzibar baada ya kutoa wanazuoni kadhaa, pamoja na kutajwa kwao kushiriki kikamilifu katika Mapinduzi ya mwaka 1964.
Kuhusu mamlaka kamili amesema suala hilo limeanza kudaiwa tangu wakati wa marehemu mzee Karume, na kwamba wanaobeza kudai mamlaka ya Zanzibar wanabeza kauli za Mzee Karume ambapo katika mkutano huo pia iliwekwa sauti ya Mzee Karume alipokuwa akitaja malengo ya Mapinduzi.
Maalim Seif aliingia Donge mapema asubuhi ambapo kabla ya mkutano huo alifanya shughuli za kuimarisha chama ikiwa ni pamoja na kufungua matawi ya Chama hicho, barza pamoja na kuweka jiwe la msingi katika tawi la CUF Donge Muwanda.
Katika Mkutano huo Maalim Seif pia alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 234, baadhi yao wakiwa wanachama na viongozi waliokihama Chama cha Mapinduzi kwa sababu tofauti, mmoja wao nd. Salim Khamis Nassor akiwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya (CCM).
sawasawa lakini afro shirazi wameuza kwa watanganyika uhuru wetu , tunaomba CUF mturudishie visiwa vyetu , tuondokane na makucha ya ukoloni mweusi , wenzetu washaanza kuchimba mafuta yao wamepeleka watu wao kusomea , sisi wanatuwekea vikwazo bado , jee mmelala fofofoooo
ReplyDeletenyinyi cuf hamkijui nini mnataka mwanzo si mlikua mnasema mapindunzi haramu na kulukua hakuna haja kufanya mapinduzi leo mnajitia kujiweka mbelle kuyatetea jiulizeni nani alikua anaunga mkino mapinduzi si mmeanza baada mroho wa madaraka seif kuingia ikulu na kukuburuzeni kwani alisemalo ndio zuri kunbe afanya kwa kujaza tumbo lake yeye anasema anataka mamlaka ya znz kunbukeni huyu mtu si ndie alomuondosha mzee jumbe madarakani alipokua anadai serikali tatu akaenda kunwambia nyerere kwa kuamini atapewa uraisi.
ReplyDeleteToa ushahidi wa nukuu ya kauli hiyo ambayo CUF iliwahi kuitoa kupinga mapinduzi. Unajisumbua tu, jahazi hilooooooo!
DeleteMaalim ikiwa Wazanzibar wanataka mamlaka kamili ,kutoka kwa nani wakati tunambia Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili zilizo ungana? Mimi hapa sijakufahamu Kuwa tazizo liko Tanganyika ijitayo Tanzania? au Tazizo liko kwa Wazanzibar wenyewe wajitao wana mapinduzi na kuiuza Dola yao ya Zanzibar kwa Sera na ilani za chama dodoma?
ReplyDeleteHujielewi lakini umo na wewe. Ule ni mkutoano wa kitaifa ambao ulifanyika Donge, kwa hiyo unawahusu wazanzibari wote. Hata CCM wenzako wana utaratibu huo huo. Kila chama kina ngome yake na kujaribu kuzitafuta ngime na mwengine. Asilia 10 ya CUF Donge si haba hebu ulizia asilimia ya CCM, Mtambwe au Pemba kwa jumla.
DeleteHawana jipwa hawa cuf, walichokisema kule donge, ispokuwa kujionesha kuwa wana magari mengi na uwezo wa kukwepa kulipa kodi. Niujanja wao, kama kweli wana kubalika ilkuwa haina haja ya kubeba watumjini kwanda nao na magari, sas maalim kawahutubia watuwa donge au wale alokwenda nao, tunajua cuf, wapo dongwe ndio mana uchaguzi uliopita walipata asilmia kumi. kura karibu masita walipata kwenye kura elfu saba
ReplyDeleteni kweli hawana jipya ..jipya unalo wewe mzee
DeleteUbovu wa cuf si uzima wa ccm kuitetea Zanzibar,wazanzibar wenyewe wanajuwa kati ya vyama hivi 2 kipi kina uzalendo wa kuitetea Zanzibar na kipi kinainakamiza Zanzibar.
ReplyDeleteMapinduzi mazumune yake nikujigomboa na zamira yake nikuwa na nchi yetu wazanzibar bila kuingiliwa .
Vipi leo tuambiwe Zanzibar sio nchi,jee kutakuwa na faida gani ya mapinduzi?
hili lina julikana maalim anawaramba visogo ndio maana wakataka kumpiga kibanda maiti kwani yy alisema hashirikiani na ccm alikua aseme ananjaa akipata kula atashirikiana na yyte hawa bwana wanajulikana walianza kutusaliti kabla ya mapinduz wakashirikiana na chama chengine wakati walishatukubalia baada ya uchaguz tutaungana ili tuunde serikal hawa wanacho wakitakacho wao na chadema hawana tofauti
ReplyDeleteKabla ya mapinduzi unazua, Maalim Seif alipiga kura yake ya Kwanza ndani ya CCM hata Afroshirazi na Hizbu hazipo tena. Seuze mimi mfuasi wa Maalim Seif ambae nilikuwa sijazaliwa. Sisi CUF ya kabla ya Mapinduzi hatukuyaona na hivyo kwetu ni historia tu wala hatufungiki na historia tunasongambele, wewe mtumwa wa historia ambayo hata ulikuwa hujazaliwa endelea kukaa katika kifungo chake. Tunataka mustakbali mwema wa nchi yetu kwetu hivi sasa, vizazi, na vijukuu vyetu na sio kabla ya Mapinduzi. Kabla ya Mapinduzi tutaendelea kuwasomesha watoto wetu historia yao kwa vitabi basi. Tanua akili utoke katika ukoloni wa Tanganyika, usidanganywe kwa kofia na fulana wewe!
DeleteSIsi tunawajua, vizuri hawa, cuf, na mtu aliyekuwa hakutoka p hata maalim, ampandishe jukwaa la zahabu, watampikaa majungu wamefanya kuwa kichaka chao, na siri iliyo mmwyoni mwao, sisi kama sisi hatutoi kisiwa hichi, wateenda donge, makunduchi, hadi bumbwin, kwa kupata serekali, cuf, washau, hawana niaa njema, na znz yetu, watuache tupumue, wanajidanganya, donge wamekenda ndio kushinda uchaguzi
ReplyDeleteHAKUNA CCM WALA CUF SASA HIVI KUNA ZANZIBAR TU
ReplyDelete