CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) Taifa jana kimepokea hundi ya Shilingi milioni tano kutoka Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikiwa ni mchango wao kwa ajili ya timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes itakayoshiriki michuano ya Chalenji yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini Kenya.
Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika huko katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, ambapo Afisa Mtendaji Silas Mwakibinga alimkabidhi hundi hiyo Katibu Mkuu wa chama hicho Kassim Haji Salum.
Akizungumza katika hafla hiyo Mwakibinga alisema kuwa msaada huo wameutoa kwa ajili ya kuendeleza umoja na mshikamano wao walionao.
Alisema kuwa Zanzibar na Tanzania Bara ni wamoja ambao wanapaswa kusaidia na kutokana na umuhimu huo wakaona ni vyema wakaichangia timu hiyo.
“Sisi na nyinyi ni wamoja na kuona tuichangie timu yetu ya Zanzibar Heroes”, alisema.
Nae Katibu Mkuu wa chama hicho Kassim Haji Salum alisema kuwa msaada huo si kama wameisaidia ZFA pekee bali wamewachangia wazanzibari wote.
Hivyo aliishukuru kamati hiyo na kusema kuwa msaada huo unafungua mahusiano mema ya ushirikiano.
Timu ya Taifa ya Zanzibar inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 24 mwaka huu, ambapo mchezo wao wa kwanza itacheza kati yao na Sudani ya Kusini.
Wanasema Msaada huo wameutoa kwa ajili yakuisaidia Zanzibar??????.. Enyi Watanganyika TIFA wacheni kuwadanganya hao Walalahoi wa Kizanzibari.. Ambao wanashuhulikia Michezo Zanzibar...
ReplyDeleteHiyo HELA muliowapatia ZAFA kwanza ni NDOGO... Kwasababu nikasema hivo hili Shirika la TAFFA Au (what ever the name) Wanapata Millioni 75 US$ kutoka FIFA ili kuimarisha Michezo Tanzania Tanganyika...
Lakini Ndio hivo tena Tuna KIVULI cha Muungano ndio Watanganyika wanapokea HELA hiyo na Kuitia Mifukoni halafu wanakuja na Millioni 5 TSh.. na Kutoa Uwongo ili Waonekane wanawapenda sana wazanzibari...
Kwanza hiyo Timu ya Taifa ya Zanzibar imejengwa na Watu Waunguja Watupu... Na wengi wao ni Wakusini au kaskazini.. Ikiwa Munataka kweli Kuunda Timu ya Taifa ya Zanzibar Jaribuni kuiga Mifano ya UK, Denmark n.k. Wachezaji wanatoka Sehemu za Mikoa au Miji tofauti iliomo UK au Denmark...
Solution znz ijitoe kwenye ujambazi wa tanganyika ili iwe member wa FIFA .hivyo tunauza fursa yetu kwa shilingi milioni tano lol akili za samaki
ReplyDelete