Habari za Punde

Kazi ya kutandikwa nyasi bandia uwanja wa Amaan kuanza wiki ijayo

Na Mwajuma Juma
KAZI ya kuanza kutandika nyasi Bandia katika uwanja wa Amaan inatarajiwa kuanza wiki ijayo baada ya kuwasili kwa Mkandarasi ambae anatarajia kufika Novemba 26 mwaka huu, akitokea nchini China.
Akizungumza na waandishi wa habari Makamo wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ)  Khamis Abdalla Said  mara baada ya kupokea nyasi hizo ambazo zinatokea nchini Kenya.
Alisema kuwa tayari juzi walizipokea nyasi hizo bandia ambazo lilitokea nchini China na sasa kilichobakia ni kumsubiri Mkarandasi ili kuanza kazi ya kulaza nyasi hizo.
“Tumepokea nyasi bandia jana (Juzi) na kazi ya kulaza itaanza mara baada ya kuwasili kwa mkarandasi”, alisema.
Aidha alisema kuwa vifaa vyengine vikavyokamilisha kazi hiyo vikiwemo gundi na Turubali litakalotumika kwa ajili ya shughuli za Kitaifa ili nyasi hizo zisiharibike zinatarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia sasa.
Nyasi hizo zimewasili visiwani Zanzibar juzi huku uwanja huo ukiwa katika hatua ya uewkaji sawa ili baadae kuweka nyasi hizo.
Uwanja wa Amaani unatarajiwa kukamilika rasmi katika wiki ya Pili ya mwezi wa Disemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.