Na Mwajuma Juma
WANAVIKUNDI wa Mazoezi wametakiwa kuandaa mazingira ambayo yatawawezesha wazazi kuwaruhusu watoto wao wa kike kushiriki katika michezo kwa kufuata mila na tamaduni zao.
Akizungumza na wanakikundi cha Mazoezi cha Kitambi Noma huko Migombani Mwenyekiti wa Michezo ya Wanawake Tanzania Irene Mwangasa alisema kuwa michezo ni afya lakini kuna vikwazo vingi hasa masuala ya utamaduni ambayo yawanawafanya watoto wakike wasiruhusiwe kushiriki katika michezo.
Alisema kuwa ndani ya Utamaduni wake wampelekee michezo mtoto wa kike lakini wasijaribu kumlazimisha avae kinyume na utamaduni wake.
“Michezo inapaswa iwe pahala salama kwa mtoto wa kike, tengenezeni mazingira ambayo yatawafanya wazazi wasiwe na wasiwasi na watoto wao”, alisema.
“Baba zangu na mama zangu nawatuma muwe mabalozi kwa kila mmoja kuiendea familia na kujaribu kuwahamasisha juu ya kumpeleka mtoto wakike katika mazoezi, mie naondoka nawatuma kila mmoja aende kwa familia moja kumuelezea kuhusu ushiriki wa mtoto wa kike katika michezo”, aliongeza.
Hata hivyo alisema kuwa Zanzibar kuna mwamko mkubwa wa watu kupenda mazoezi tofauti na na Tanzania Bara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi hicho Suleiman Mohammed Rashid amesema kuwa suala la uhuni na hulka ya mtu na sio kwa kushiriki katika michezo.
Kikundi hicho cha Mazoezi cha Kitambi Noma nimkikundi mama kati ya vikundi zaidi ya 50 vilivyopo hapa Zanzibar vinavyoshiriki mazoezi.
No comments:
Post a Comment