Habari za Punde

Balozi Seif aridhishwa na ukarabati wa Ikulu ndogo ya Kibweni

 Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Nd. Salum Maulid akimtembeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika baadhi ya sehemu za nyumba ya Ikulu ndogo iliyopo Kibweni Wilaya ya Magharibi.


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwaagiza wahudumu wa Ikulu ndogo ya Kibweni kuhakikisha kwamba mazingira ya nyumba hiyo yanaendelea kuwa mazuri.



Jengo la Ikulu ndogo iliyopo Kibweni Wilaya ya Magharibi ambalo linatarajiwa kuhudumia baadhi ya wageni watakaoalikwa kuhudhuria sherehe za Maadhimisho ya Kutimia Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame, OMPR

Taasisi inayosimamia uhifadhi na matengenezo ya nyumba za Serikali imeshauriwa  kuifanyia marekebisho yaliyosalia Ikulu ndogo ya Kibweni ili itumike vyema katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar  ya mwaka 1964.

Ushauri huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alipofanya ziara fupi ya kuikagua nyumba hiyo  iliyopo pembezoni mwa Makao Makuu ya Kikosi cha kuzuia Magendo Zanzibar { KMKM } Kibweni Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi.

Balozi Seif ameridhika kiasi na hali halisi ya mazingira ya Ikulu hiyo alisema ni vyema   nyumba hiyo ya Serikali  ikapangiwa taratibu za kutumika badala ya kuachwa ikikaa bure .

Alisema Serikali katika kipindi kirefu imekuwa ikipokea wageni wa Kitaifa na Kimataifa wenye hadhi ya kuishi kwenye nyumba hiyo lakini wengi kati yao wanaishia kuwekwa  katika Hoteli  za Kitalii jambo ambalo linaweza kuepukwa.


Aliwataka wahusika wa matengenezo ya nyumba za Serikali  kuhakikisha kwamba nyumba  hiyo { Ikulu } inakamilishwa hitilafu  ndogo ndogo zilizobakia ili iweze kuhudumia wageni watakaoalikwa kuhudhuria maadhimisho ya  sherehe za Mapinduzi kutimia Nusu Karne.

“ Tunatarajia kupokea wageni wengi wa Kitaifa na Kimataifa katika sherehe zetu za mwaka ujao . Hivyo kwa hadhi ya nyumba hii tunaweza baadhi yao kuwapangia wakampumzika kwa kutwa moja kabla na baada ya sherehe zetu kabla hawajarejea nyumbani “. Alisisitiza Balozi Seif.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  aliwapongeza wasimamizi wa Ikulu hiyo ya Kibweni kwa hatua  wanazozichukuwa katika kuihudumia nyumba hiyo kongwe.

Alisema mazingira bora yaliyopo hivi sasa kwenye nyumba hiyo  yanaruhusu kwa baadhi ya Mikutano na Kazi za  Viongozi Wakuu wa Serikali  kuzifanyiwa katika eneo hilo.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Nd. Salum Maulid alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba tatizo liliopo hivi sasa katika nyumba hiyo ni  marekebisho ya jiko la kupikia pamoja na huduma ya maji ambayo haipatikani kikawaida.

Nd. Salum alisema huduma hiyo ya maji safi   hupatikana kwa nadra katika kipindi kirefu tatizo ambalo linahitaji kufanyiwa utafiti wa kina na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.



2 comments:

  1. Wallahi hawa CCM wanajua kupoteza pesa za wazanzibari... jengo ndani limewekwa Masofa ya Kifaghari lakini mishahara ya madaktari, walimu na wafanyakazi wa SMZ hairidhishi hata kidogo...

    hata hivyo hio Ikulu ndogo kwanini isiwekwe makumbusho... ? Tupatieni hiyo thamani ya matumizi ili tuweze kulinganisha na matengenezo yenyewe... siajabu huyo katibu amershakula chake hapo ndio akawa anaburura tumbo.

    ReplyDelete
  2. Hawaoni hata aibu kutumia, pesa za walipakodi, kukarabati nyumba kufanyia ufuska, usalama wataifa, angalau, wangaikarbati wkaifanya makumbusha, watalii kwakenda kujionea histaria, kwnye hili jengo,

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.