Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Kenya na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo Ijumaa January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete ambaye alitua nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia alifariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto na balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda Buriani walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete, aliyetua Nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia alifariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete, aliyetua Nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia alifariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.(Picha na Ikulu )
Uteuzi wa Bi Saada Mkuya, SMZ inatakiwa ijifunza kuteuwa W'bari wenye vipaji ktk nafasi za muungano na sio kupeleka 'vimeo'
ReplyDeleteNadhani kwa sasa kila mtu ameona kua 'ukipanda mahindi , utavuna mahindi' huyu dada ana uwezo wa aina yake, hadi watu wanajiuliza kama kweli Z'bar kuna watu wa aina yake!
sio kweli ndugu yangu , huyu kapewa ili kujaribu kutuliza presha za watu wasiotaka muungano , pamoja na mwinyi kupewa ulinzi , lakini msimamo ule ule hatutaki muungano hata mkitupa wizara zote kuwa waznz mawaziri , hao mawaziri wetu si chochote bali ni sawa na mbuzi waliotiwa kamba ya shingo , hawana hili wala lile , waandishi wa habari ni marafiki wa wanasiasa wakitaka watakufanya uonekane shujaa au adui kwa siku moja tu bila kujali wewe ni mwema au adui kikweli
ReplyDelete